Waziri
wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja (kulia) amekutana na
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bw. Alberic Kacou ofisini
kwake jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuelekea Dodoma ambapo
vikao vya Bunge vinaendelea.
Waziri
wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja (kulia)akiteta jambo na
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bw. Alberic Kacou ofisini
kwake jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuelekea Dodoma ambapo
vikao vya Bunge vinaendelea.
Mh.
Ngeleja amekutana na Mwakilishi huyo baada ya kuwasili kutoka katika
mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaohusu Nishati
uliofanyika nchini Ubelgiji.
Mh.
Ngeleja aliiwakilisha Tanzania katika sekta ya Nishati ambapo Umoja wa
Mataifa unategemea Nishati kuwafikia watu wote ifikapo Mwaka 2030.
Mh.
Ngeleja amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo haswa upatikanaji wa
fedha, Serikali ya Tanzania imedhamiria kusambaza nishati nchini
Tanzania (yenye watu zaidi ya milioni 45) kutoka asilimia 18.5 hadi
asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.
Naye
Mwakilishi wa Umoja wa Matifa amemshukuru Waziri kwa jitihada zake
kupitia wizara hiyo na akasisitiza kuwa Nishati kwa kila mtu ni haki ya
msingi hivyo uharakishwaji wa mpango huo wa nishati kwa wote upewe
umakini mkubwa.
Pia
ameahidi kufikisha maombi ya Waziri wa Nishati ikiwa ni pamoja na
kuondolewa vikwazo vya upataji wa fedha kwa nchi zinazoendelea ikiwemo
Tanzania kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon.
Kusoma zaidi: www.tz.one.un.org
Imetolewa na
Ofisi ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa
Afisa Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)