Warembo wa kitongoji cha Ukonga wenye tisheti za orange na wale wa
Tabata wenye tisheti za blue katika pozi mara baada ya ya Miss Tabata
kutembelea kambi ya MIss Ukonga
Miss Ukonga wakionyesha utaalamu wao
Mmoja ya warembo wa Miss Tabata akipita jukwaani
Waratibu wa TAbata na Ukonga wakibadilishana Mawazo.
WAREMBO
wa vitongoji viwili vya Ukonga na Tabata jana walifanya mazoezi ya pamoja katika
kuleta ushirikiano na kujenga urafiki baina ya warembo hao katika fani ya
urembo.
Warembo
wa Tabata waliwatembelea wenzao wa Ukonga katika kambi yao ya mazoezi iliyopo
Ukonga Hill Tech Bar maeneo ya Minazi Mirefu au maarufu Banana.
Vitongoji
vya Ukonga na Tabata warembo wake watakao shinda wanataraji kukutana katika
Kambi ya kanda ya Ilala kabla ya kwenda kushiriki shindano la taifa la Miss
Tanzania 2012.
Wakizungumza
jana baadhi ya warembo wa Ukonga wamesema ushirikiano wao huo na wenzao wa
Tabata unawapa uwezo wa kijiamini na kupata nafasi ya kujifunza kile ambacho
wenzao wanakifanya au wamejifunza ikiwa ni pamoja na utembeaji, uongeaji wa kati
wa kujitambulisha na vitu vingine vingi.
“Tunawashukuiru
sana waandaji wetu, maana mbali ya kuwa tunapata wageni wa aina mbalimbali ambao
ni wadau wa urembo lakini leo tupo na washiriki wenzetu wa tabata ambao
tunaimani tutakutana katika shindano la Ilala”, alisema Amina Sangawe.
Nae
Suzanne Deodatus ambaye ni Mshiriki kutoka Tabata alisema wamepata fursa ya
kujifunza mambo kabdhaa na wamefurahi sana kuwatembelea warembo wa Ukonga na
kufanya nao mazoezi ya pamoja.
Mapema
Mwezi huu warembo wa Ukonga waliwasindikiza Miss Tabata 2012 katika show yao
kubwa ya Utambulisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar West Tabata.
Shindano
la Miss Ukonga 2012 linataraji kufanyika Mei 5, mwaka huu na lile la Tabata
linataraji kufanyika mapema mwezi Juni.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)