Ananilea Nkya Mkurugenzi Mtendaji Tamwa
---
Viongozi
wa mashiriki matatu yanayotetea haki za wanawake na watoto wamesema
ni muhimu wananchi mijini na vijijini wakaanza kujadili madhara ya
ulevi na kuchukua hatua kuepusha vitendo vya ukatili
vinavyosababishwa na ulevi.
Wamesema bila jamii kuchukua hatua madhubuti kupambana na ulevi nchi itaendelea kushuhudia vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyokosesha familia amani ambayo ni msingi muhimu wa maendeleo ya familia na taifa.
Wamesema wanaume wanaokunywa pombe na kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wanaweza kubadilika endapo wananchi katika ngazi za vijiji, mitaa na kwenye taasisi wangeanzisha mjadala kuhusu namna bora ya kupambana na ulevi.
Viongozi hao kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Shirika la Haki za Wanawake – KIVULINI na Kituo cha Usuluishi (CRC) walisema hayo walipokuwa wakizungumza na TAMWA kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki.
Wamesema kwa mfano matukio mengi ya wanawaume kuwapiga wake zao, ubakaji, lugha za kudhalilisha utu, na wazazi kutohudumia watoto kwa kuwapatia chakula, mavazi na elimu yanachangiwa na ulevi.
Maimuna Kanyamala, Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI ambalo linaendesha kampeni ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake katika kanda ya Ziwa amesema kupitia sinema na mijadala ya umma wanaume zaidi ya 350,000 katika kanda hiyo wamebadilika na familia zao zinaishi kwa amani.
Amesema watu hao waliweza kuacha pombe baada ya kuona sinema iliyoonyesha mambo maovu ambayo mtu anaweza kufanya kutokana na kunywa pombe.
Mkurugenzi wa WLAC Theodosia Muhulo Nshala na Mratibu wa CRC Elizabeth Muhangwa wamesema wanawake wengi na watoto wanaofika katika mashirika yao kutaka msaada wa ushauri na wa kisheria ni wale ambao wamefanyiwa ukatili ambao kwa namna moja au nyingine umechochewa na unywaji wa pombe. Viongozi wa mashirika hayo wameyataka mashirika yote ya kijamii yanayotoa msaada wa kisheria na ushauri kwa wanawake na watoto kuchunguza kwa kina mashauri wanayopokea ili kufahamu ni yepi yana uhusiano na pombe.

Wamesema kwa kufanya hivyo nchi itaweza kupata takwimu sahihi kuhusu ni kwa kiasi gani unywaji pombe unavyochangia ukubwa wa tatizo la ukatili wa kijinsia.
Imetolewa na:
Ananilea Nkya
Mkurugenzi Mtendaji Tamwa
Mkurugenzi Mtendaji Tamwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)