Profesa
Chris Peter Maina wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
akielezea na kufafanua umuhimu wa Mahakama, akitolea mfano ya ICTR
kushirikiana na Taasisi na Mashirika ya Kijamii katika kuhakikisha haki
inatendeka, haswa katika matukio kama ya uhalifu wa kivita, wakati wa
Kongamano la kimataifa lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo.
Baadhi
ya Wanafunzi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wakisikiliza Lecture ya Profesa Chris Peter Maina wakati wa mjadala
wawazi wa kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari
yaliyotokea nchini Rwanda Mwaka 1994.
Ofisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Stella Vuzo,
akisoma hotuba kwa niaba ya Mshauri Mwandamizi wa Mahakama ya Kimataifa
ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda, ambapo amehimiza nchi
washiriki kuwa na imani na mahakama ya ICTR.
Mmoja
kati ya wanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
akichangia mada katika mjadala wawazi kuhusiana na madhara na nini
tujifunze kutokana na mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini
Rwanda.
Mwanafunzi
wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichangia mada
katika mjadala wawazi kuhusiana na madhara na nini tujifunze kutokana na
mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.
***************************
***************************
Na.Mwandishi wetu.
Wananchi wa Rwanda na Afrika Mashariki kwa Ujumla wametakiwa kulinda na kudumisha amani katika eneo la maziwa makuu kwa kuwa hiyo ndio misingi ya umoja amani na maendeleo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Msemaji na Mshauri Mwandamizi wa Kisheria wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda Bw. Roland Amoussouga, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vizo, amesema mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita nchini Rwanda inasikitika na inatoa pole kwa wale walioathiririwa na vita vilivyotokea mwaka 1994na kuwa iko pamoja nao.
Aidha amesema tunapaswa kuweka kumbukumbu ya waliopoteza maisha na walionusurika , ambao kwa sasa wameathirika kimwili na kiakili.
Katika kongamano la kimataifa lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)