Mgombea
nafasi ya Makamu wa Urais wa Seikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha
Tumaini-Iringa (TUSO-IUCO) Judith Kahwa akimwaga sera zake.
Mgombea
nafasi ya Urais wa Seikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa
(TUSO-IUCO) Mchungaji Joshua Chusi akimwaga sera zake.
Mgombea
nafasi ya Urais wa Seikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa
(TUSO-IUCO) Mauna Chuma Belius akimwaga sera zake.
KAMPENI
za Uchaguzi Mkuu wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa
(IUCO) zinazidi kupamba moto huku wagombea mbalimbali wakipita kunadi
sera zao katika madarasa, Hostel na maeneo mbalimbali chuoni hapa.
Viongozi
hao wanaowania nafasi mbalimbali za kuiongoza Serikali ya Wanafunzi
chuoni TUSO-IUCO wanafanya kampeni hizo tayari kwa uchaguzi baada ya
kipindi cha uongozi wa Serikali iliyipo madarakani kumaliza muda wake.
Serikali
iliyopo madarakani chini ya Rais wake Method Kagoma inafikia ukomo wake
kesho Aprili 21, 2012 baada ya kufanyika uchaguzi mkuu.
Taarifa
kutoka Tume ya Uchaguzi Chuoni hapo inasema watakaokuwa na sifa ya
kupiga kura hiyo kesh ni wanafunzi wote halali wa Chuo hicho cha Tumaini
Iringa.
Aidha
Tume hiyo inasema kuwa Mwanafunzi halali ni Yule aliye na kitambulisho,
hivyo asiye na kitambulisho atakosa haki yake ya msingi ya kupiga kura
kuchagua viongozi wake katika uchaguzi huo.
Nafasi
zinazowaniwa katika Uchaguzi huo ni pamoja na nafasi ya Rais, Makamu wa
Rais, pamoja na wawakilishi wa Vitivo (wabunge) na wawakilishi wa
Maeneo (Madiwani) ambao wote watapigiwa kura hiyo kesho.
Wagombea
mbalimbali wamekuwa wakipita hapa na pale ikiwa ni pamoja na kubandika
picha zao katika kuta ikiwa ni sehemu ya kutafuta kura.
Orodha kamili ya wagomfuatavyo.
Wagombea nafasi ya Urais ni Mauna Chuma,Joshua Chussy na Henericus Kanyaruju ambapo nafasi ya Makamu wa Rais ni
Judith Kahwa,Elizabeth Invocaviti na Albin Msechu.
Kitivo
cha Sanaa wagombea ni Hilton John na Paul Osujack, wanaowanania nafasi
saidizi ni Evans Boniface na Anwar Ahmed wakati wagombea wa Kitivo cha
Sheria ni Nkumbuke Yongolo na Kassile Kassile na wasaidizi ni Luciano
Nyengo.
Kitivo
cha Uchumi wagombea wake ni Godfrey Gaitano na Godfrey Kaziri ambapo
wagombea wa Kitivo cha Education niVivian Msafiri na Godfrey Komu huku
wasaidizi wao ni Willford Chale.
Wagombea wa Kitivo cha Theologia ni Willium Nkuhi na Aziz Mchomvu wakati wagombea wasaidizi ni Sifuni Makongwa.
Wagombea
nafasi ya Urais ni Mauna Chuma,Joshua Chussy na Henericus Kanyaruju
ambapo nafasi ya Makamu wa Rais ni Judith Kahwa,Elizabeth Invocaviti na
Albin Msechu.
Kitivo
cha Sanaa wagombea ni Hilton John na Paul Osujack, wanaowanania nafasi
saidizi ni Evans Boniface na Anwar Ahmed wakati wagombea wa Kitivo cha
Sheria ni Nkumbuke Yongolo na Kassile Kassile na wasaidizi ni Luciano
Nyengo.
Kitivo
cha Uchumi wagombea wake ni Godfrey Gaitano na Godfrey Kaziri ambapo
wagombea wa Kitivo cha Education niVivian Msafiri na Godfrey Komu huku
wasaidizi wao ni Willford Chale.
Wagombea wa Kitivo cha Theologia ni Willium Nkuhi na Aziz Mchomvu wakati wagombea wasaidizi ni Sifuni Makongwa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)