UHABA WA MAJI WAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA NTYUKA MKOANI DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

UHABA WA MAJI WAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA NTYUKA MKOANI DODOMA

Maji bado ni tatizo hususani katika Mkoa wa Dodoma  ambapo wakazi wengi wa Mkoani Dodoma hususani maeneo ya vijijini hupata maji ambayo siyo safi na salama kama ambavyo kijana huyu ambaye hakupenda jina lake kuchorwa mtandaoni  alipokutwa na Mtandao wa Lukaza Blog akiwa ametoka kuchota maji kwaajili ya matumizi ya nyumbani kwao maji yenyewe ndo ayo kama yanavyoonekana. Kijana Huyu anaishi Maeneo ya Ntyuka Mbali kidogo na Dodoma Mjini ndani ya Manispaa ya Dodoma.

Akiongea na Mtandao wa LUKAZA blog, kijana huyu alisema kuwa achilia mbali umbali wanaokwenda kuchota maji bali hata maji wanayoyapata sio safi na salama katika matumizi ya binadamu lakini kwasababu ni Shida basi hawana budi Kuchota na kutumia  japokuwa wanajua kuwa maji hayo ambayo sio safi na salama huweza kuleta magonjwa lakini huwa wanamuachia Mungu Kwa Kulinda Maisha Yao.

Aliongezea Kwa Kusema Kuwa tokea azaliwe hajawahi kuona maji ya bomba yanafananaje na kusema kuwa ameshazoea maji hayo na hayajawahi kumletea madhara yoyote yale
Picha NaShax Ngeta Wa Lukaza Blog.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages