RPC wa Kinondoni-Charles Kenyela |
POMBE
kali (Whisky) aina ya Jacky Daniel, imetajwa kama chanzo cha kifo cha
mwigizaji nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba aliyefariki
usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amesema leo kwamba uchunguzi
wa awali unaonyesha hivyo, lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi,
ili kujua zaidi.
ACP
Kenyela amesema kwamba Kanumba wamefanikiwa kumuhoji mtuhumiwa wa
kwanza katika tukio hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na katika maelelezo
yake amekanusha kumsukuma Kanumba.
Vyombo
vingi vya habari vilimnukuu ndugu wa Kanumba, Sethi jana akisema kwamba
Lulu alimsukuma mwigizaji mwenzake huyo katika ugomvi wao wa wivu wa
kimapenzi hadi akaanguka na kufariki dunia.
Akizungumza
kutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda huyo alisema kwamba; ugomvi wao
ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati akizungumza na simu.
“Kanumba
aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti, akitaka aelezwe kwa
nini alitoka nje kupokea simu, huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa
akizungumza na mwanaume mwingine.
Baada
ya Lulu kuona Kanumba anamfuata, aliamua kukimbia kutoka nje ya geti,
lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba alimkamata na
kumrudishwa ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani
na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa
maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,”alisema
Kamanda huyo.
Akiendelea
kumnukuu Lulu, Kamanda huyo anasema; “Baada ya Kanumba kufunga mlango,
alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho
kabla ya kuanguka chini,”alisema.
Alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.Kwa Hisani ya Father Kidevu Blog
Tunashukuru brother Lukaza, blog yako inavutia siku hadi siku kwa habari motomoto.
ReplyDeleteendelea kutupa raha tunakuaminia.
Carol
Thanks for good good news lukaza blog, keep it up
ReplyDeletecarol