Wakili
wa waleta maombi Wanaccm Godfrey Wasonga akitafakari kwa hisia kali
muda mfupi kabla ya kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ubunge Tundu Lissu
hayajatangazwa.
Mbunge
wa jimbo la Singida mashariki CHADEMA),Tundu Lissu,muda mfupi baada ya
mahakama kuu kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na Shaban Selema na
Pascal Halu wa CCM,kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge.
Mbunge
wa jimbo la Singida mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu akifutwa machozi na
mke wake wakati wakitoka nje ya mahakama baada ya mahakama kuu
kutangaza kuwa ushindi wake huo,ni halali.
Baadhi
wa watu waliohudhuria kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi
yaliyompa ushindi Tundu kuwa mbunge muda mfupi baada ya maamuzi hayo
kutolewa.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mbunge
wa jimbo la Singida mashariki (CHADEMA)Tundu Lissu imeigaragaraza
vibaya CCM baada ya mahakama kuu kutupilia mbali hoja 11
zilizowasilishwa na waleta maombi wawili wanachama wa CCM za kutaka
kutengua ushindi wake wa ubunge kwa madai kuwa, alikiuka sheria na
taratibu za uchaguzi na kusababisha uchaguzi huo kutokuwa huru na wa
haki.
Shabani
Selema na Pascal Halu wote wanachama wa CCM na wakazi wa kijiji cha
Makiungu tarafa ya Mungaa jimbo la Singida Mashariki, walifungua kesi ya
kupinga matokeoa yaliyompa ushindi Tundu kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Jaji
Mosses Mzuna wa makahama kuu Moshi mjini mkoa wa Kilimanjaro, katika
kutoa hukumu hiyo, amesema ushahidi uliotolewa na upande wa waleta
maombi, umeshindwa kuthibitisha bila kuacha shaka yo yote kuwa,
mlalamikiwa wa kwanza, wa pili mwanasheria mkuu wa serikali na wa tatu
msimamizi wa uchaguzi, kuwa walivunja/kiuka sheria, taratibu na kanuni
za uchaguzi na kusababisha uchaguzi huo kutokuwa huru na wa haki.
Akitoa
maamuzi ya makahama, amesema kuwa katika hoja zote 11 zilizoletwa na
waleta maombi hao, ushahidi wote ni wa kuhisi, kusikia na kushuku,
ambao hauna uhalisia wa mambo yaliyowasilishwa.
Jaji
Mzuna amesema kuwa mahakama yo yote haiwezi kutegua matokeo ya uchaguzi
kwa kuambiwa maneno matupu bila ya maneno husika kuthibishwa kwa
‘document’ husika.
Amesema ushahidi wa upande wa walalamikaji pia umekuwa ni kama kinyonga, mara kwa mara ulikuwa ukukigeuka geuka.
Akifafanua
zaidi, Mzuna ametaja baadhi ya hoja ambazo zililetwa na waleta maombi
kuwa ni mlalamikiwa Tundu kuandaa barua tano zinazofanana kwa mawakala
wa CUF, TLP, AAPT Maendeleo, NCCR -Magezui na CHADEMA, kwa lengo la
kujinufaisha katika zoezi la uchaguzi mkuu.
Ametaja
hoja nyingine kuwa Tundu aliwapa chakula mawakala wa chama chake na wa
vyama vingine isipokuwa wa chama cha CCM, kitendo ambacho kiliashiria ni
hongo ili mawakala wasiokuwa wa chama chake nao wampigie kura.Habari Kwa Hisani ya MO Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)