TASWIRA ZA MADUKA TISA YALIYOUNGUA KWA MOTO STENDI KUU YA ARUSHA MUDA MFUPI ULIOPITA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TASWIRA ZA MADUKA TISA YALIYOUNGUA KWA MOTO STENDI KUU YA ARUSHA MUDA MFUPI ULIOPITA

 Askari wa Kikosi cha kuzima moto jijini Arusha wakijaribu kuzima moto huo bila mafanikio.
 Moshi mkubwa ukiwa umetanda angani kutokana na moto huo.
Umati wa watu ukisangalia moto aliokuwa ukiunguza maduka jijini Arusha leo.PICHA NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA

Na Gladness Mushi  wa Fullshangwe-ARUSHA

WANANACHI  wa jiji la Arusha wameomba serikali kuongeza zaidi vifaa kwa kikosi cha zima moto ijini hapa kwa kuwa mara nyingi sana kikosi hicho kinashindwa kuokoa wananchi katika majanga ya moto kutokana na kutokuwa na vifaa vya kutosha yakiwemo maji

Wakizungumza na Waandishi wa habari  jijii hapa katika tukio la kuungua kwa maduka tisa yaliyopo Stendi ya mkoa  katika  mtaa wa majengo wananchi hao walisema ukosefu wa maji ya kutosha kwa kikosi hicho unachanmgia sana maafa na kwa hali hiyo Serikali inatakiwa kuliangalia hilo

Walisema kuwa mara nyingi sana kikosi hicho cha kuzima moto kinafima kwa ajili ya kuokoa  bidhaa  pamoja na maisha ya watu ambao wamenusurika na ajali za moto lakini wanashindwa kufanya kazi zao

Wananchi hao walifafanua kuwa endapo Kama hali hiyo ya uzembe itaendelea basi kikosi hicho kitakuwa hakina faida kwa wananchi, na hali hiyo inatakiwa kudhibitiwa mara moja kwa ajili ya kuokoa maafa ya ajali za moto

Walisema kuwa katika tukio hilo la kungua kwa maduka kama tisa ya biashara mbalimbali ambalo lilitokea majira ya saa tisa za mchana katika mtaa wa majengo  stendi kubwa walisema kuwa  magari yaliokuwa na maji yalifika kwa muda muafaka lakini hawakuwa na maji ya kutosha

Wananchi hao walisema kuwa iwapo kama Magari hayo ya Fire yangekuwa na maji ya kutosha basi ni wazi kuwa kwa kiwango kikubwa sana wangeweza kuokoa maduka hayo dhidi ya moto mkubwa

Katika hatua nyingine Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Bw Akili Mpwapwa alibitisha kuungua kwa maduka hayo tisa na kusema kuwa chanzo bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages