Waandishi wa habari za uchunguzi juu ya masuala ya ukatili
wa kijinsia (GBV) kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika
ofisi za TAMWA jijini Dar es Salaam kabla ya safari ya kuelekea mikoa
mbalimbali kufanya kazi hiyo (Picha na Thehabari.com)
Na Thehabari.com-
Dar es Salaam
CHAMA cha
Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimeteua baadhi ya waandishi wa habari za
uchunguzi masuala ya ukatili wa kijinsia (GBV) kwa lengo la kuwapeleka katika
mikoa 20 ya Tanzania Bara na Visiwani kuandika habari za ukatili wa kijinsia
kwa wanawake na watoto.
Akizungumza
mapema jana jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na wanahabari hao,
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Ananilea Nkya amesema jumla ya wanahabari 18
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wanakwenda kufanya kazi hiyo, ambapo
wamepangiwa wilaya moja kwa kila mkoa.
Amesema
wanahabari hao pamoja na mambo mengine wanakwenda kufanya uchunguzi juu ya
habari za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto vitendo ambavyo vimekuwa
vikishamiri katika maeneo kadhaa ya nchi, huku vikikandamiza haki anuai za
msingi dhidi ya jamii hiyo.
Bi. Nkya alisema
uchunguzi huo utafanyika ndani ya siku 14 katika vijiji kadhaa, huku wanahabari
wakifuatilia kwa kina vitende vya ubakaji, ukeketaji, vipigo kwa wanawake,
utelekezaji familia pamoja na wanafunzi kukatishwa masomo na kuozeshwa.
Ameitaja mikoa ambayo waandishi wamepelekwa na wilaya zake
kwenye mabano ni pamoja na Morogoro (Mvomero), Mtwara (Newala), Shinyanga
(Kahama), Dar es Salaam (Ilala, Temeke na Kinondoni), Kilimanjaro (Same), Pwani
(Mkuranga), Mara (Tarime), Manyara (Simanjiro), Tanga (Handeni), Kigoma
(Kasulu), Iringa (Kilolo), Mbeya (Rungwe), Singida (Iramba), Dodoma (Kondoa), Arusha (Karatu), na Njombe
(Njombe).
Kwa upande wa Zanzibar mikoa
ambayo waandishi watafanya kazi hiyo ni pamoja na Kaskazini Pemba
(micheweni na Wete), Kusini Pemba (Chakechake), Kaskazini Unguja (Kaskazini A
na B, Kusini Unguja (Kusini Unguja) na Mjini Magharibi (Wilaya ya Kati).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)