Spika Wa Bunge Anne Makinda Akutana na Wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki Kutoka Tanzania Waliochaguliwa na Bunge jana Mjini Dodoma - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Spika Wa Bunge Anne Makinda Akutana na Wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki Kutoka Tanzania Waliochaguliwa na Bunge jana Mjini Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowasa (Mb) akifafanua jambo kuhusu utendaji kazi wa Bunge la Afrika Mashariki na Bunge letu wakati wa kikao kati ya Spika na wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania waliochaguliwa na Bunge jana. Wabunge hao walikutana na Mhe. Spika kwa lengo la kufahamiana pamoja na kupewa maelezo ya awali kuhusu mahusiano ya Bunge letu na Bunge la Afrika Mashariki.
Makamu Mwenyekiti Kamati ya Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akiwaeleza jambo wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki wakati wa kikao kati ya Spika na wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania waliochaguliwa na Bunge jana. Wabunge hao walikutana na Mhe. Spika kwa lengo la kufahamiana pamoja na kupewa maelezo ya awali kuhusu mahusiano ya Bunge letu na Bunge la Afrika Mashariki.
Mmoja wa wabunge waliochaguliwa kwenye Bunge la Afrika Mashariki,akichangia mada kwenye mkutano huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (kulia) akiwa katika kikao cha pamoja na wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania waliochaguliwa na Bunge jana. Wabunge hao walikutana na Mhe. Spika kwa lengo la kufahamiana pamoja na kupewa maelezo ya awali kuhusu mahusiano ya Bunge letu na Bunge la Afrika Mashariki.
Wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania waliochaguliwa na Bunge jana wakimsikiliza kwa Makini Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (hayupo pichani) wakati alipo kutana nao kwa lengo la kufahamiana pamoja na kupewa maelezo ya awali kuhusu mahusiano ya Bunge letu na Bunge la Afrika Mashariki.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages