Balozi
mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Sano Lambert (kushoto) akisalimiana
na Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda Bw. Roland
Amoussouga.Katikati ni Afisa habari wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji
ya Kimbari Rwanda Bw. Danford Mpumilwa.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella
Vuzo akimkaribisha ukumbini Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji
ya Rwanda Bw. Roland Amoussouga wakati sherehe za maadhimisho ya miaka
18 ya Kimbari leo jijini Dar es Salaam.
Balozi
mdogo wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Sano Lambert akizungumza kwa niaba
ya serikali ya Rwanda kuhusu maadhimisho ya mauaji ya Kimbari na
kushukuru serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wanaoutoa kwa nchi yake
baada ya mauaji ya hayo ya mwaka 1994.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya nchi za nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mh. Mahadhi Juma Maalim akitoa hotuba rasmi ya kuadhimisha Mauaji ya
Kimbari na kuwahakikishia Wanyarwanda kwamba Serikali ya Tanzania
itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali ya Rwanda.
Msemaji
wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda Bw. Roland Amoussouga
akitoa hotuba yake ya Maendeleo ya Kesi za mauaji ya Kimbari nchini
Rwanda katika maadhimisho hayo leo jijini Dar es Salaam. Bw. Roland alisema kati ya kesi 92 za mauaji ya Kimbari 83 zimeshasikilzwa.
Mkurugenzi
Mwakilishi wa shirika la kazi Duniani (ILO) Bw. Alexio Musindo
akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa katika
maadhimisho ya miaka 18 ya mauaji ya Kimbari Rwanda leo jijini Dar es
Salaam.
Afisa
habari wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari Rwanda Bw.
Danford Mpumilwa akimuonesha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya nchi
za nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim mabango
mbalimbali ya kukumbuka mauaji ya Kimbari ya Rwanda wakati maadhimisho
ya miaka 18 ya Kimbari jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule mbalimbali wakisoma mabango na machapisho mbalimbali ya kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda.
Tukio la kuwasha mishumaa kuwakumbuka waathirika wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika mwaka 1994.
Mabalozi na wawakilishi mbalimbali wa Umoja wa Mataifa wakifuatilia hotuba ya Mh. Mahadhi Juma Maalim.
Mh. Zitto Kabwe (wa kwanza kushoto) alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)