SBL KUBADILISHA MAISHA YA WATEJA WAKE! 'Yazindua Promosheni ya ‘Vumbua Hazina chini ya kizibo’ - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SBL KUBADILISHA MAISHA YA WATEJA WAKE! 'Yazindua Promosheni ya ‘Vumbua Hazina chini ya kizibo’

 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw. Ephraim Mafuru akitangaza rasmi mbele ya waandishi wa habari promosheni kabambe ya vinywaji vya kampuni hiyo inayoitwa Vumbua Hazina chini ya Kizibo, ambapo zaidi ya shilingi milioni 700 zitashindaniwa zikiwemo fedha, pikipiki, Bajaji na Magari manne.

Bia zitakazohusika katika promosheni hiyo ni Pilsner Ice, Tusker Lager na Serengeti Lager na watu watashiriki promosheni hiyo kupitia kwa kutuma ujumbe wa namba zilizopo katika vizibo vya bia hizo kupitia mitandao mbalimbali na kupokea zawadi zao kupitia M-Pesa baada ya kushinda. Promosheni hiyo inaanza jumanne Aprili 24.
Katika picha kulia ni Mtaalam wa Bidhaa SBL Bw. Maurice Njowoka na kushoto ni Asia Natalia MhinaMkuzaji wa Biashara ya M-Pesa kutoka Vodacom Tanzania.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw. Ephraim Mafuru akielekeza zawadi zitakazoshindaniwa katika promosheni hiyo kulia ni Asia Natalia MhinaMkuzaji wa Biashara ya M-Pesa kutoka Vodacom Tanzania na katikati ni Mtaalam wa Bidhaa SBL Bw. Maurice Njowoka.
 Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Wadau ktoka kampuni ya Push Mobile wakiwa katika mkutano huo.
 Wadau kutoka kampuni ya R&R wakipozi kwa picha.
Wadau kutoka kampuni ya bia ya SBL wakiwa katika picha ya pamoja.


Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia vinywaji vyake bora kabisa vya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager iameandaa promosheni kubwa na ya aina yake itakayofanyika Tanzania nzima katika kipindi cha wiki 16 ambapo zawadi mbalimbali zitashindaniwa.
Promosheni hiyo ya aina yake imesheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile Jenereta 16 , Pikipiki 8, Bajaji 8, Gari ndogo maarufu kama saloon car 8, pamoja na zawadi zingine nyingi ambapo kila baada ya wiki mbili gari 1  aina ya saloon itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki mbili Bajaji 1 itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki  Pikipiki moja itashindaniwa na kila baada ya wiki moja Jenereta moja itakuwa inashindaniwa.

Akizungumzia promosheni hiyo  kabambe Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, bwana Ephraim Mafuru amesema  promosheni hiyo sio tu inalenga kuongeza mauzo ya vinywaji hivyo bali pia inalenga kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania hususani wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ikiwa ni sera mojawapo ya kampuni hiyo kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia bidhaa zake zenye ubora wa aina yake.

“Kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya taifa letu katika maeneo mbalimbli kupitia jamii inayotuzunguka na wateja wetu kimaisha, hivyo promosheni hii pamoja na ukweli kuwa inalenga kuongeza tija katika masoko ya bidhaa zetu bado unaweza kuona zawadi zitakazoshindaniwa katika promosheni hii ni zawadi kubwa ambazo kwa namna moja ama nyingine inaweza kubadilisha maisha ya mshindi wetu kutoka hatua aliokuwepo hadi hatua nyingine, kwa hivyo sisi SBL tunasema tunajivunia kuwa sehemu mojawapo inayochangia maendeleo ya watanzania wateja wetu na taifa kwa ujumla” alisema bwana Mafuru. 
 
Kwa upande wake Meneja wa bia ya Tusker Lager, Bi Rita Mchaki, amesema kampuni ya bia ya Serengeti inazalisha bidhaa zinazopendwa na watanzania wengi kutokana na ubora wa kipekee wa bidhaa hiyo, na kwamba promosheni hiyo kabambe nisawa nakurudisha shukrani zake kwa watanzania kwa kufanikisha kampuni hiyo kufikia malengo yake kibiashara.  
 
Watanzania wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi na wanaotumia bidhaa zetu zilizoainishwa katika promosheni hii wanaombwa kushiriki kwa wingi bila kukata tamaa kwani zawadi zinazoshindaniwa zinaweza kubadilisha maisha kwa yeyote atakayebahatika kuibuka na ushindi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages