Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu
Brigedia Jenerali Mstaafu
Adam Mwakanjuki mapema asubuhi leo April 22, 2012
katika kambi ya JWTZ ya Kikosi cha Anga kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi

Mwili ukipelekwa kwenye Ndege
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za
rambirambi Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha
mwanasiasa mkongwe Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki aliyefariki dunia
katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo jijini Dar-es-Salaam jana tarehe 19
April, 2012.
Marehemu amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi visiwani Zanzibar zikiwemo za Uwaziri katika Wizara mbalimbali na pia kuwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
"Pokea rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na mzee wetu, kiongozi shupavu na mwanamapinduzi imara, ni pengo kubwa kwetu kwani Marehemu amekuwa mshauri wetu mkweli na muwazi, upendo na ucheshi wake pia ilikuwa faraja kwetu wakati wa vipindi vigumu na vyepesi" Rais ameeleza,
"Tutaukosa ushauri wake, upendo wake na mchango wake katika kila hali" Rais amesema na kumuomba Rais Dk. Ali Mohamed Shein kufikisha salamu zake za rambirambi kwa familia, wananchi wote na viongozi wenzake ambao marehemu amefanya nao kazi katika idara zote serikalini, jeshini, na pia katika Baraza la Wawakilishi.
Marehemu Mwakanjuki alianza Siasa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 akianzia katika Chama Cha Afro Shiraz (ASP) na baadae Chama cha Mapinduzi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi
Jenerali Davies Mwamunyange na Mh Aboud wakiangalia wakati jeneza lenye mwili
wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki ulipokuwa
unaingizwa katika ndege mapema asubuhi leo April 22, 2012 katika kambi ya JWTZ
ya Kikosi cha Anga kabla ya kupelekwa Zanzibar
kwa mazishi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)