Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkuu wa Jeshi la akiba nchini Brigedia
Generali R.M Muhuza hayupo pichani katika ofisi yake leo alipomtembelea
kujitambulisha na kueleza juu ya ujio wake Mkoani Rukwa ambapo ni kuona
matayarisho ya kikosi cha mgambo cha Mkoa wa Rukwa ambacho kitashiriki kwenye
zoezi la kijeshi litakalohusisha Vikosi vya JWTZ vilivyopo katika Mikoa ya
Nyanda za Juu Kusini (Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa, Lindi, Mtwara, Njombe na
Katavi) ifikapo tarehe 15 Septemba 2012. Zoezi hilo la kijeshi litaandaliwa na
Brigedi ya 401 KV iliyopo Songea Mkoani Ruvuma. Jumla ya Wanamgambo 60 kutoka
Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kushiki zoezi hilo litakalojumuisha vikundi toka
Kamandi zingine za Ndege za Kivita, Wahandisi, Mizinga na
Vifaru.
Kutoka kushoto ni
Mkuu wa Jeshi la akiba nchini Brigedia Generali R.M Muhuza, Msaidizi wake Kanali
A.Y Amasi na Katibu wake Meja A.R Gumbo kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi
wa Tanzania Dar es Salaam wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa walipomtembelea
Ofisini kwake leo.
Mazungumzo
yakiendelea.
Miongoni mwa mambo aliyosisitiza Mkuu huyo wa Mkoa
ni uboreshwaji wa sekta muhimu nchini kama sekta ya ulinzi ili kuepusha uvunjifu
wa amani iliyodumu nchini kwa muda mrefu. Alisema Jeshi la Wananchi lina jukumu
kubwa la kuhakikisha amani inakuwepo nchini na sio kutokana na hatari zinazoweza
kutoka nje bali kwa hatari zinazoweza kusababishwa na wananchi
wenyewe. (Picha na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa RUKWA"rukwareview.blogspot.com " )
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)