Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akimsalimu mke wa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete alipokwenda kuwasalimia
katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo.
Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akimpa Rais Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya jezi ya timu ya Democrata anayofundisha nchini Brazil alipokwenda kumsalimia Rais katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo.
Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akisalimiana na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete alipokwenda kumsalimia Rais katika hoteli ya
Tivoli jijini Sao Paulo.PICHA NA IKULU
Na Anna Nkinda – Sao Paul, Brazil
18/04/2012 Vilabu vya soka nchini vimeshauriwa kuwa na timu nzuri kuanzia ngazi ya watoto wenye umri wa miaka nane, vijana na kuendelea ili kupata timu bora ya Taifa.
Wito huo umetolewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Star Marcio Maximo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Sao Paul.
Maximo
alisema kuwa timu nyingi ambazo ni bora na zinafanya vizuri katika
mchezo wa soka zimekuwa zikiwaandaa watoto wenye vipaji vya mchezo huo
wangali wadogo ili waweze kuwa wachezaji wazuri hapo baadaye.
Kocha
Maximo pia alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho
kikwete, ambapo alimnshukuru sana Rais kwa ushirikiano wa hali ya juu
aliompa wakati alipokuwa akiifundisha Taifa Stars miaka takriban mitatu
iliyopita.
Kwa
upande wake Rais Kikwete alimpongeza Kocha Maximo kwa juhudi zake za
kuendeleza soka la Tanzania, akimwambia uwepo kwake Tanzania kuliasidia
sana kuiweka nchi katika ramani ya mchezo huo.
Rais
Kikwete alikubaliana na kocha huyo kwamba ili timu ya Taifa ifanye
vyema ni lazima maandalizi yaanzie ngazi za chini, ikiwemo vilabu kuwa
na timu za watoto na vijana ambao baadaye watakuwa hazina ya Taifa
Stars.
Kuhusiana na uvumi ulioenea kuwa anataka kwenda
kufundisha timu za Taifa Stars, Azam na Yanga alisema kuwa siyo kweli
na wala hajawasiliana na timu hizo na hawezi kwenda kufundisha kwani hivi sasa anamkataba wa kufundisha timu ya Democrata iliyopo nchini humo.
Rais
alimshukuru Kocha Maximo kwa kuja kumsalimia na kumpa zawadi ya jezi ya
timu ya Democrata anayofundisha, na kumtakia heri na fanaka katika kazi
yake hiyo.
“Timu
ya Taifa Star ina kocha mzuri ambaye ninamuheshimu na ninaukubali
ufundishaji wake hivyo basi kupitia kocha huyo ninaamini watanzania
watazidi kuendelea katika soka na kufika mbali zaidi”, alisema.
Maximo alimalizia kwa kusema kuwa anamawasiliano mazuri na watanzania na anawapenda ndiyo maana kila mahali anapopita anajivuna na kusema kuwa Tanzania ni nchi yake ya pili.
Hivi sasa Maximo ni kocha wa timu ya Democrata
iliyopo nchini humo ambapo wiki ijayo inatarajia kuanza mashindano ya
taifa yatakayopelekea kupata wachezaji bora watakaoshiriki mashindano
ya kombe la Dunia yanayotarajia kufanyika mwaka 2014 nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)