Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake
wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na
Utafiti yaliyoanza leo Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Simon Shayo, wakati
alipotembelea katika Banda la Chuo Kikuu cha DUCE cha jijini Dar es
Salaam, alipofika kuzindua maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu
na Utafiti yaliyoanza leo Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee. Kushoto ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo hicho, Abdul
Njaid.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Ardhi, Prof.
Mangisen Kaseva, wakati alipotembelea katika Banda la Chuo hicho baada
ya kuzindua maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu na Utafiti
yaliyoanza leo Aprili 18, 2012 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kulia
ni Ofisa Utawala wa Chuo hicho, Rosemary Bundara.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na baadhi ya wafanyakazi wa
TCU, baada ya kufungua rasmi maonyesho ya Vyuo Vikuu na Taasisi za
Elimu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo, Aprili 18, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)