Makamu
wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na wanamichezo wa Ikulu, wakati akiwaaga na kuwatakia
ushindi
wakielekea kushiriki katika Bonanza maalum la Pasaka linaloanza leo,
katika Viwanja vya Sigara (TCC Chang’ombe) jijini Dar es Salaam. Makamu
alikutana na wanamichezo hao wa Ikulu ya Zanzibar na Dar es Salaam, leo
asubuhi
Ikulu ya jijini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na wanamichezo wa Ikulu, (hawapo pichani) wakati akiwaaga na
kuwatakia ushindi kuelekea kushiriki katika Bonanza maalum la Pasaka linaloanza
leo, katika Viwanja vya Sigara (TCC Chang’ombe) jijini Dar es
Salaam. Makamu alikutana na wanamichezo hao wa Ikulu ya Zanzibar na Dar es
Salaam, leo asubuhi Ikulu ya jijini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Ikulu, Peter Ilomo (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi
ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mwinyiusi Hassan.
Baadhi
ya wanamichezo wafanyakazi wa Ikulu, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akizungumza nao kuwapa
Baraka za ushindi wakielekea kushiriki katika Bonanza maalum la Pasaka.
Baadhi
ya wanamichezo wafanyakazi wa Ikulu, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akizungumza nao kuwapa
Baraka za ushindi wakielekea kushiriki katika Bonanza maalum la Pasaka.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana
na baadhi ya Wafanyakazi na wanamichezo
wa Ofisi za Ikulu ya Dar es Salaam na Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo
nao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi ‘wanamichezo’ Ikulu za Zanzibar na
Dar es Salaam, wanaoelekea kushiriki Bonanza la Pasaka, baada ya mazungumzo nao
Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)