Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na
Kiongozi wa Timu ya Madaktari Bingwa 16 wa Cuba Dr. Freddy Fagindo mara
baada ya kuwasili kwa ajili ya chakula cha pamoja.
Kushoto yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Juma Duni Haji.
Kiongozi wa Madaktari Bingwa wa Cuba wanaotoa huduma za afya hapa
Zanzibar Dr. Freddy Fagindo akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake baada
ya kuandaliwa chakula cha usiku na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi hapo Nyumbani kwake Mazizini.
Kulia ya Dr. Freddy ni Waziri wa Afra Mh. Juma Duni Haji na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika
Picha ya pamoja na Madaktari Bingwa wa Cuba wanaotoa huduma za afya hapa
Zanzibar baada ya kumaliza chakula cha pamoja hapo nyumbani kwake
Mazizini.
---
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Serikali ya Cuba kwa uwamuzi wake wa
kuendelea kusaidia kuiunga mkono Zanzibar katika masuala ya Huduma za
Afya.
Pongezi hizo amezitoa hapo nyumbani kwake Mazizini wakati akizungumza
na Madaktari Bingwa wa Cuba wanaotoa huduma za Afya Nchini baada ya
kumaliza nao chakula cha pamoja cha usiku.
Balozi Seif Alisema Zanzibar hivi sasa imepiga hatua kubwa ya Maendeleo
katika huduma za Afya ambapo Cuba ina mchango mkubwa na wa muda mrefu
wa Utaalamu katika fani hiyo.
Alisema Afya ni miongoni mwa sekta ziliyopewa msukumo mkubwa na
Serikali katika Sera ya kuwa na Kituo cha Afya kwa kila masafa ya
Kilomita Tano Unguja na Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba sera hiyo
inatarajiwa kwenda sambamba na mpango wa Wizara ya Afya wa Kuwapatia
Taaluma Madaktari wazalendo 50 Chini ya Wataalamu wa Cuba.
“ Kundi hili la Madaktari 50 Wazalendo wanaofunzwa na Walimu wa Cuba
litasaidia kupunguza uhaba wa Madaktari liliopo hapa Zanzibar”.
Alisisitiza Balozi Seif Ali Iddi.
Aliowaomba Madaktari hao kujihisi kwamba huduma wanazozitoa zinafanana
na zile walizokuwa wakizitoa Nchini kwao na Serikali itakuwa tayari
kushirikiana nao ili lile lengo lao la kuwepo Zanzibar liweze kufanikiwa
.
Naye Kiongozi wa Madaktari hao 16 Kutoka Nchini Cuba Dr. Freddy Fagindo
alisema yeye na Timu yake wameelezea furaha yao kutokana na ukarimu
mkubwa wanaoupata kutoka kwa Wananchi wa Zanzibar.
Dr. Freddy alimuhakikishia Balozi Seif kwamba Taaluma pamoja na huduma
wanayoitoa itawafikia Walengwa ambao ni Wananchi walio wengi.
Kiongozi huyo wa Timu ya Madaktari wa Cuba ambae kituo chake kipo Mjini
Dar es salaam alieleza kwamba Sera za Cuba ni kuona Taaluma iliyomo
ndani ya Nchi hiyo inasambaa katika maeneo inayohitajia popote pale
Duniani.
Na
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)