Aliyekua Mbunge wa Arusha Mjini,(CHADEMA)Mh Godblesss Lema
---
MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.
Taarifa
kutoka jijini Arusha zinasema uamuzi huo umefikiwa leo asubuhi Aprili
5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel
Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la
Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).
Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buruiani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).
Lema katika Uchaguzi huo alikuwa akichuana vikali na Mgombea wa CCM, Dk. Batilda Salha Buruiani ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya.
Kuvuliwa
Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado chama hicho kipo
katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki
mkoani humo.
Pia
habari za ndani ya Chama cha Chadema zinasema kuwa tayari Chama hicho
kilisha soma alama za nyakati mapema katika kesi hiyo miezi kadhaa
nyuma na kujipanga endapo mbunge huyo atavuliwa wadhifa wake nani
kimsimamishe kutetea kiti hicho.
Habari
hizo zinadai kuwa Chadema kimepanga kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chama
hicho na Mgombea Urais wa 2010, Dk. Wilbroad Silaa kutetea kiti hicho.
Wanachama hao
wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa wa kuwa
mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya
kampeni aliyofanya jimboni Arusha.
Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5 kujitetea.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)