Mshambiliaji
wa timu ya Barcelona Fc, Lionel Messi, akipiga Penati wakati wa mchezo
wa mzunguko wa pili wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya yao na
Chelsea mchezo uliochezwa jana, kwenye Uwanja wa Nou Camp Barcelona.
Baada ya timu hizo kutoka droo ya 2-2 Chelsea imeibuka kidedea kuendelea
na fainali hizo ikiwa na jumla ya mabao 3-2 dhidi ya Barcelona.
Fernando Torres wa Chelsea alipokua akishangilia goli lake la pili dhidi ya Barcelona katika raundi ya pili ya nusu fainali ya uefa champion ambapo barcelona ilifungashiwa virago kwa kufungwa jumla ya magoli 3 kwa 2
Fernando Torres akishangilia goli lake la pili na mchazaji mwenzake wa Chelsea Didier Drogba wakati wa Mechi ya raundi ya pili ya Nusu fainali ya UEFA dhidi ya Barcelona mchezo uliomalizika kwa droo ya kufungana magoli 2 kwa 2 na kupelekea Barcelona kufungashiwa vilago kwa goli moja la ziada
Mesi na Cesc Fabregas akiwa hajui la kufanya baada ya timu yake kufungasha virago katika nusu fainali dhidi ya Chelsea na Barcelona mechi iliyochezwa jana Katika Dimba la Camp Nou jijini nchini Hispania
Nahodha wa Chelsea John Terry alipopewa Kadi nyekundu katika mchezo huo dhidi ya Barcelona lakini fernando torres alipeleka furaha nchini Uingereza Kwa kuifunga Barcelona Goli la Pili na Kuifanya Barcelona Kuaga Mashindano hayo ya UEFA champion league
Messi Akisalimiana na Frank Lampard wakati timu hizo zinakwenda mapumziko huku Barcelona Ikiwa Mbele kwa Magoli 2 kwa 1
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)