Vijana
wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Ofisa Mwandamizi wa
Makao Makuu ya CCM, Gordon Mwakitabu kuliingiza nyumbani kwa marehemu,
eneo la Area C, mjini Dodoma kwa ajili ya kuaga na mazishi
yaliyofanyika baadaye kwenye makaburi ya Nkhungu nje kidogo ya mji.
Aliyebeba msalaba ni mtoto wa kwanza wa marehemu Mwakitabu, Martin
Mwakitabu
Katibu
Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (katikati) akizungumza na makatibu wakuu
wastaafu wa CCM, Philip Mangula (kushoto) na Yussuf Makamba, wakati wa
shughuli za maziko ya aliyekuwa Ofisa Mwandamizi Makao Makuu ya CCM,
Gordon Mwakitabu mjini Dodoma
Mjane
wa Gordon Mwakitabu, Janeth Mwakitabu akiangua kilio wakati wa kuaga
mwili wa marehemu mumewe, nyumbani kwao, Area C, mjini Dodoma
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Mwakitabu wakati wa kuaga
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akiaga mwili wa marehemu mwakitabu
Makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Philip Mangula wakiuaga mwili wa marehemu Mwakitabu
.
Waombolezaji wakiwa katika huzuni na mshangao, wakati wa kuaga mwili wa
marehemu Mwakitabu. Waliokaa mbele, Kutoka Kushoto ni Katibu wa NEC,
Mambo ya Nje, Januari Makamba, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)