Alice Foundation yawakumbuka watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Alice Foundation yawakumbuka watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi

Mwenyekiti wa Alice Foundation, Alice James Dosi wakitoa maelekezo kwa atoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi katika Kata ya Ubungo wakati Taasisi hiyo, ilipowandalia hafla jijini Dar es Salaam jana. Zaidi ya Watoto 400 walishiriki katika hafla hiyo ambapo waliweza kufanya michezo mbalimbali kula na kunywa pamoja kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo.
Taasisi ya Alice yenye makazi yao eneo la Sinza jana iliandaa hafla kwa watoto waishio katika mazingira magumu waishio katika kata ya Ubungo ambapo pia iliwakutanisha watoto hao na wengine waliopo shuleni.

Akizungumza na Elimubora Mkurugenzi wa Alice Foundation, alisema kuwa hafla hiyo inalenga kuwaweka pamoja watoto waishio katika mazingira magumu kuwafariji na kuwapati ushauri nasaha.

Alisema kuwa watoto 400 walishiriki hafla hiyo iliyoshirikisha michezo mbalimbali kama vile kuvuta kamba, mbio za mayai katika kijiko, kunywa soda, kupokezana vijiti, kukimbia na magunia.

Alisema kuwa watoto walifurahia tukio hilo na alisisitiza kuwa litakuwa likifanyika mara kwa mara.

Taasisi hiyo ya Alice inajishughulisha pia na masuala ya utunzaji wa mazingira, uwezeshaji wa akina mama, haki za wanawake, kusaidia watoto waishio mazingira magumu na  masuala ya Mkukuta.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages