Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi moja kati ya
kompyuta 20 zilizotolewa na Airtel kwa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa
Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula (kulia) juzi wakati
wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika chuoni hapo. anaeshuhudia
ni Mkuu wa wilaya ya Bahi Bi Betty Mkwasa (kati). Airtel imetoa
vitabu 104 na computer 20 vyote vina thamani ya milioni 25/- TZS ikiwa
ni muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi baadhi ya vitabu vya
chuo kikuu vilivyotolewa na Airtel kwa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula (kulia) juzi
wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika chuoni hapo. Anaeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi Bi Betty Mkwasa (kati). Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote vyenye thamani ya milioni 25/- TZS ikiwa ni muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Makamu
Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM) Profesa Idrisa Kikula (katikati)
akiwashukuru Airtel mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya wanafunzi
wa chuo hicho juzi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104
na kompyuta 20 vyote vyenye thamani ya milioni 25/- TZS kutoka Airtel
ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini. Kulia
ni mkuu wa wa wilaya ya Bahi Betty Mkwasa na toka shoto ni Meneja
Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Mkuu
wa wilaya ya Bhahi Mheshimiwa Betty Mkwasa akiongea na waandishi wa
habari na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho juzi wakati wa hafla fupi
ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye thamani ya milioni 25/- TZS toka
Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Anaefuata ni Makamu mkuu wa chuo hicho profesa idrisa Kikula na
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Mkuu
wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa, akiwa na Makamu Mkuu wa chuo cha
Dodoma (UDOM) juzi pamoja na wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya
wanafunzi wa IT chuoni hapo wakiwa wameshikilia vitabu vilivyotolewa
msaada na Airtel kwa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya
vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye thamani ya milioni 25/- TZS toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote
vyenye thamani ya milioni 25/- TZS kwa chuo kikuu cha Dodoma ikiwa ni
muendelezo wa shughuli zake za kijamii katika kuchangia sekta ya Elimu
nchini.
Komputa
hizo pamoja na vitabu vimekabidhiwa kwa Makamu Mkuu wa chuo cha UDOM
kilichopo mkoani Dodoma jana wakati wa hafla fupi iliyofanyika ukumbi
mdogo wa mikutano chuoni hapo na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya
Bhahi Mh, Betty Mkwasa
Akiongea
wakati wa makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya wa Bhahi aliishukuru
Airtel Tanzania kutokana na jitihada zake za kushirikiana na serikali
katika kusaidia sekta mbali mbalimbali ikiwemo elimu
“Hili
ni tukio muhimu sana mnalofanya Airtel na inaonesha dhahiri dhamira
yenu ya kushirikiana na serikali yetu na jamii kwa ujumla kuchangia
elimu ili kuinua kiwango cha elimu nchini, hivyo kufanya hivi nchi yetu
inafaidika sana”
“ninawaomba
wanafunzi kuhakikisha mnavitumia kikamilifu kompyuta na vitabu hivi
ili kujiongezea ujuzi na uelewa zaidi katika masomo kwa manufaa yenu na
kwa taifa pia” alimaliza kusema Mh Mkwasa
Nae
Meneja uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema” Airtel chini ya
mpango wetu maaalum wa kuchangia elimu bado tutaendelea kuchangia
elimu nchini, leo tunaona fahari sana kuweza kujitolea sehemu ya faida
yetu pia kwa taasisi ya elimu ya juu (UDOM), msaada wetu huu wa
kompyta 20 na vitabu 104 vya elimu ya juu ni muendelezo wa mpango wetu
wa *Airtel Shule Yetu *uliodumu kwa zaidi ya miaka saba ukiwa ni
maalum kwa kuchangia elimu
“kwa
kupitia mpango wa Airtel Shule yetu tumeshanikiwa kuzifikia zaidi ya
shule 800 na kutoa msaada wa vitabu na vifaa vya kufundishia yakiwemo
pia madawati”
Kwa
mwaka 2012-2013 bado Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia
sekta ya elimu katika nyanja tofauti ikiwapo; kutoa madawati kwa shule
za msingi na sekondari, kurekebisha majengo ya shule, kutoa computer
kwa shule za sekondari na vyuo lengo hasa likiwa ni kushirikiana na
serikali katika kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu bora ili kuweza
kupata nguvu kazi ya kesho na kulikomboa taifa katika swala la
umaskini na elimu duni.
Nae
Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM) Profesa Idrisa Kikula
aliishukuru Airtel na kuongeza kuwa msaada huo wa kompyuta na vitabu
umeenda wakati muafaka na unahitajika sana.
“Vitabu
na komputa hizi ni muhimu kwa chuo kikuu chetu cha Dodoma, tunaamini
kabisa vitabu hivi vitasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa
vitabu na zaidi kuwapatia wanafunzi na walimu nyenzo za kujisomea na
kufundishia pia” alisema Profesa Idrisa Kikula Makamu mkuu wa chuo UDOM
“Msaada huu umekuja muda muafaka kwa kuwa Komputa ni muhimu sana kwa elimu ya
juu ukizingatia karne hii ya sayansi na teknololojia hivyo zitatumika
kufundishia masomo mbalimbali ya ICT na kuwapa wanafunzi ujuzi wa
teknolojia ya habari na sayansi ya kompyuta” alimaliza kwa kusema
Profesa Idrisa Kikula Makamu mkuu wa chuo UDOM
Chuo
kikuu cha Dodoma ambacho ni maarufu kama UDOM kilifunguliwa rasmi
mwaka 2007 huku kikiwa na sifa ya kuwa na maabara kubwa (library)
kuliko chuo chochote cha elimu ya juu kilichopo nchini. Kwa sasa chuo
hicho kinakadiriwa kuhudumia zaidi ya wafunzi 20,000 nchini huku
matarajio ni kufikisha wanafunzi kutoa elimu kwa wanafunzi 40,000 kwa
siku zijazo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)