Wanahabari
Iringa wakiwa katika maandamano ya amani ya kupinga manyanyaso kutoka
ofisi ya mkuu wa mkoa Iringa.Picha na Habari na Mdau Francis
Godwin-iringa
--
MAANDAMANO
ya wanahabari mkoa wa Iringa leo yatikisa mji wa Iringa baada ya
wananchi kusitisha shughuli zao na kushiriki kuunga mkono maandamano
hayo makubwa ya aina yake mkoani Iringa.
Katika
maandamano hayo yaliyopita mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa ikiwa ni
pamoja na stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoni wasafiri walishuka katika
mabasi waliyokuwa wakisubiri kuanza safari na kuungana na wanahabari
hao kwa kusindikiza kwa muda maandamano hayo .
Wakitoa
maoni yao juu ya maandamano hayo baadhi ya wananchi akiwemo Maneno
Mbuma na mzee Said Sanga walisema kuwa hofu ya mkuu wa mkoa wa Iringa
kupokea maandamano hayo haikupaswa kuwepo kutokana na utulivu na hekima
ya hali ya juu iliyoonyeshwa na wanahabari hao.
Mbuma
alisema kuwa jamii ya mkoa wa Iringa haipotayari kuendelea kukosa haki
yao ya msingi ya kupata habari kwa ubaguzi na manyanyaso ya ofisi ya
mkuu wa mkoa wa Iringa dhidi ya wanahabari na kuwa vyombo vyote vya
habari vinapaswa kupewa haki sawa ya kuhabarisha umma juu ya matukio
yanayotokea katika mkoa.
Hivyo
alisema kama kweli ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa haikuwa na matatizo
hayo ambayo wanahabari wameamua kuyapinga basi mkuu wa mkoa Dkt
Christina Ishengoma angekubali kupokea maandamano hayo ya amani ila
kukimbia kupokea maandamano hayo ni sawa na kuogopa ukweli dhidi ya
ofisi yake.
Huku
Sanga akimtaka mkuu wa mkoa wa Iringa kulegeza msimamo wake na kukaa
chini na wanahabari hao ili kujenga mahusiano mema badala ya kuendelea
kujenga daraja kati ya ofisi yake na vyombo vya habari.
Akipokea
maandamano hayo ya wanahabari zaidi ya 60 wa vyombo mbali mbali mkoani
Iringa mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC)
ambao ndio walidhamini maandamano hayo ya wanahabari mkoani hapa ,Daud
Mwangosi alisema kuwa wengi wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya
maandamano hayo huku baadhi ya watu wakidhani wanahabari hao
wanaandamana kwa ajili ya kutetea kulipwa posho na baadhi wahusisha
maandamano hayo na itikidi za kisiasa na kuwa maandamano hayo hayakuwa
na mitazamo hiyo kama wanavyofikiri bali ni maandamano ya kupinga
manyanyaso dhidi ya wanahabari na ubaguzi dhidi yao.
Pia
alitaka wanahabari mkoani Iringa kutokubali kuendelea kunyamaza kimya
kwa ubaguzi unaofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa pamoja na
ofisa habari wa ofisi hiyo Denis Gondwe
Alisema
kuwa IPC itaendelea kuwaunga mkono wanahabari katika kupinga vitendo
vyote vya ukandamizaji na manyanyaso kwa wanahabari katika mkoa wa
Iringa na kuendelea kuungana na vilabu vya wanahabari kute nchini
ambavyo havipo tayari kunyanyaswa na vyombo vya umma na kumwima haki yao
ya kutoa habari ama kupata habari.
Mwangosi
pia amewapongeza viongozi wa vilabu vya wanahabari mkoa wa Mbeya,
Ruvuma , Arusha na mikoa mingine ambayo imetoa tamko la kuunga mkono
maandamano hayo ya wanahabari likiwemo jukwaa la wahariri hapa nchini
kwa kutoa msimamo wao wa kuunga mkono maandamano hayo ya amani ya
kupinga wanahabari kunyanyaswa na kuutaka muungano wa vilabu vya
wanahabari Tanzania (UTPC) kushiriki kupinga manyanyaso kwa wanahabari
pia.
Katika
hatua nyingine wanahabari hao mkoani Iringa wametangaza msimamo wao
iwapo mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Ishengoma hatajibu madai yao na
kuendelea na msimamo wake wa kupuuza madai ya wanahabari hao basi hawata
kuwa tayari kushirikiana na ofisi yake .





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)