Muonekano
wa nje wa Royal bakery mara baada ya Camera ya Jiachie ilipowasili eneo
la tukio usiku huu na kukuta difenda ya polisi kutoka kawe ikiwa
imewasili eneo hilo,wakati huo huo kukiwa na heka heka za hapa na pale. kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa bakery hiyo.
Askari
wa kituo cha Kawe,wakichukua maelezo kwa baadhi ya wafanyakazi wa
bakery hiyo,namna tukio lilivyokuwa,mmoja wa wafanyakazi aliyenaswa
vibao akilia kwa uchungu.
Masikini Dada wa watu akilia kwa uchungu,huku polisi wakiendelea kuchukua maelezo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Bakery hiyo wakiwa wameduwaa wasijue la kufanya kwa
muda huo mara baada ya majambazi kupora kiasi cha fedha ambazo haikuweza
kubainika mara moja ni kiasi gani mpaka Camera ya Jiachie inaondoka
eneo la tukio usiku huu.
********
********
Kwa
mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Royal Bakery hiyo ameeleza kuwa tukio
la kuvamiwa na majambazi eneo hilo imetokea mnamo majira ya saa 3 na
ushehee hivi (usiku huu),anasema majambazi hao walikuwa watano
waliwasili eneo hilo wakiwa na piki piki mbili na gari. Mmoja aliyekuwa
ameshika bastola aliingia ndani na kuwaamuru wafanyakazi waliokuwemo
ndani wote walale chini,na kuanza kuchukua fedha za mauzo zilizokuwemo
kwenye droo zao za kuhifadhia fedha,huku wengine nje wakifyatua risasi
hewani na kufunga barabara kwa muda wa dk 10 hivi.
Dada
huyo aliyejikuta akiangua kilio wakati akielezea,anasema kuwa yeye
amepigwa pigwa makofi na hakujeruhiwa,kama vile haitoshi anasema kuwa
eneo hilo pia kulikuwepo na wazungu wapatao watatu ambao walienda pale
kujipatia huduma mbalimbali,kwa bahati mbaya wakakutana na dhahma
hiyo,ambapo nao walilazwa chini na kuporwa wallet zao sambamba na pete
zao walizokuwa wamevaa mikononi,baada ya ambush hiyo majambazi
wakatoweka kusikojulikana ndipo difenda ya polisi ikawasili na kuanza
kuchukua maelezo kadhaa Picha na habari kwa hisani ya Jiachie Blog









I like the valuable info you provide in your articles. I will bookmark your blog and check again here regularly. I’m quite sure I will learn many new stuff right here! Best of luck for the next!
ReplyDeleteThank You
RNB Research
thanks na nafarijika kuona kuwa kazi yangu pia inawafikia wahusika na wanaisoma nasema asante na nitaendelea kuongeza juhudi katika kazi ili ziweze kuwafikia na wengine wengi na nasema karibu kila siku kwa kutembelea blogu hii na naomba uwe balozi mzuri tu kwa wengine na kuwataarifu juu ya hii blogu asante sana na kazi njema
Delete