Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taaria ya Mkoa toka kwa Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama mara tu baada ya kuwasili Ikulu ndogo
mjini Moshi jioni hii.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipokewa kwa furaha
walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hiitayari kwa ziara ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa furaha mara alipotua uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hii. Kulia ni Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama.PICHA NA IKULU
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili
mjini Moshi jioni ya leo, Jumapili, Machi 4, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku
tatu.
Miongoni mwa
shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya
kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa
kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.
Shughuli hiyo
itakayofanyika kesho Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la
Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Mbali na
kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa
Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.
Hii ni ziara
ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea
Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
MWISHO
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILINO YA RAIS
MARCH 4, 2012
MOSHI





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)