Rais
Jakaya Kikwete akifungua maji ya bomba kuashiria uzinduzi rasmi wa
mradi wa maji katika kijiji cha Itunundu kata ya Pawaga Iringa
uliogharimiwa na kanisa la Anglican Dayosisi ya Luaha Mkoani Iringa kwa
zaidi shilingi bilioni mbili, Huku wakuu wa kanisal hilo wakishuhudia,
kutoka kulia ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Luaha Dornald Mtetemela,
Martha Mgomi Mratibu wa mradi huo na Askofu Joseph Mgomi wa Daayosisi ya
Luaha.
FULLSHANGWE ilikuwepo katika msafara
huo na kukuletea taswira mbalimbali za kuwasili kwa Mh. Rais Jakaya
Kikwete pamoja na shughuli yake ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji
cha Itunundu kata ya Pawaga mkoani Iringa.
Rais
Jakaya Kikwete akimpongeza mama Agnes Msavi mara baada ya kumtwisha
ndoo ya maji kuashiria ukombozi kwa mwanamke kutokana na kukamilika kwa
mradi huo.
Warembo
wa kimasia wakiwmlaki Rais Jakaya kikwete huku wakiwa wameshikilia
bendera za taifa alipowasili katika kijiji cha Itunundu.
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Kamanda wa vijana mkoani Iringa Salim
"Sas" Abri mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mjini
Iringa.
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Askofu wa Dayosisi ya Luaha Joseph Mgomi
wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mjini Iringa leo
mchana, kushoto ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Luaha Dornald
Mtetemela.
Rais Jakaya Kikwete akiwatunza wasanii wa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza wakati alipowasili mjini Iringa leo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)