Hapa akionyesha mautundu katika Tumba, pembeni yake ni Victor Nkambi na Msafiri Diouf
Kija akimwangalia kwa makini Nape akipiga gitaa la Bass!
Nape Nnauye akipiga Drums huku Msafiri Diouf akiimba
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye leo alipata fursa ya kipekee
kujiunga na Bendi ya Twanga Pepeta "Kisima Cha Buruduni" na kufanya nao
mazoezi ndani ya ofisi za Aset. Baada ya kufanya makamuzi ya nguvu
ilidhihirika wazi kwamba ukiachilia mbali siasa Nape ni msanii mkali wa
kuimba, na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki. Aidha Mkurugenzi wa Aset
Asha Baraka alifurahishwa na kumshukuru sana Nape kuja kuwatembelea na
kuwapa sapoti, vilevile alimuahidi kuwa nafasi yake itakua wazi kwenye
bendi mara tu atakapo amua kuachia ngazi kutoka katika jukwaa la siasa
na kuamua kujiunga katika tasnia ya muziki.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)