Msanii
wa Muziki kutoka nchini Afrika ya Kusini, Cleopas Monyepao (DJ Cloe)
(kulia) akizungumza na waandishi wa habari, Dar es salaam leo kuhusu
onyesho lake litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama
kesho. Kushoto ni Msanii aliyeongozana naye, Dumiseni Mkihanya.
Na Mwandishi Wetu
CLEOPAS
Monyepao maarufu kama DJ Cleo mkali wa nyimbo ya Facebook kutoka Afrika
Kusini kesho anatarajia kutoa burudani katika viwanja vya Posta,
Kijitintama jijini Dar es Salaam.
Dj
Cleo ameambatana na wachezaji wake Dumisani Makihanya 'Bleksem' na Dj
Soul T ambaye amekuwa akionekana katika video mbalimbali za nyimbo zake.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Dj Cleo alisema
amefurahishwa sana na ujio wake hapa nchini ikiwa ni mara yake ya
kwanza na hiyo ni kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi
hizi mbili.
Alisema, anaamini katika onesho lake hilo la kesho atajifunza mengi kutoka kwa wasaniiwakali wa hapa nchini na Watanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kufanya shoo katika jukwaa moja na wanamuziki wa Bongo na kujua utamaduni wa Mtanzania kupitia sanaa.

Aliongeza
kuwa anahitaji sana kujifunza utamaduni wa Tanzania kwani nchi hizo
zinaushirikiano mkubwa na zinaendana kwa mambo mbalimbali kwa kiasi
kikubwa ikiwa ni pamoja na muonekano wa wananchi wake.
Aidha alisema, kwa upande wa burudani atawapa mashabiki burudani nzuri na ambayo wataridhika nayo ingawa mashabiki wake wengi wa Tanzania wanaujua wimbo wake wa Facebook kwa sana kuliko nyingine, lakini yeye ananyimbo nyingi hivyo zitakuwa ni 'Supries' kwao.
"Watu wengi wanaujua wimbo wangu wa Facebook lakini zipo nyimbo nyingi tu ambazo ni nzuri, ambazo zitakuwa ni mpya kwao na ninaamini watazipenda hivyo waje kwa wingi ili waweze kujionea na kusikia," alisema.

Naye
kwa upande wake mmoja wa wanamuziki ambao wataimba jukwaa moja na DJ
Cleo, Omari Nyembo 'Ommy Dimpoz' alisema, anajisikia faraja kubwa
kupanda jukwaa moja na msanii huyo kwani anaimani naye atajifunza mengi
kutoka kwa msanii huyo.
Alisema, kupanda jukwaa moja na wasanii wa nje kunawasaidia muziki wao kufahamika Kimataifa zaidi kwani utajulikana ukilinganisha kazi yake hasa mwanamuziki huyo ni ya Udj.
Alisema, kupanda jukwaa moja na wasanii wa nje kunawasaidia muziki wao kufahamika Kimataifa zaidi kwani utajulikana ukilinganisha kazi yake hasa mwanamuziki huyo ni ya Udj.
Sambamba
na wanamuziki hao pia jukwaa hilo litapambwa na Suma lee, Dully Sykes,
Juma Nature, Tip Top Conection, Wanaume Halisi, Chege na Temba, Wanaume
TMK na Wakali Dancers

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)