Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein,akisalimiana na Viongozi na watendaji katika viwanja vya Ukumbi wa
Salama Bwawani Hotel, alipohudhuria katika mkutano wa majumuisho ya
ziara aliyoifanya katika wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
mwishoni mwa wiki hii, ili kuangalia maendeleo ya sekta mbali mbali za
Kijamii.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein,akizungumza na Viongozi na watendaji wa Wilaya ya Mjini Mkoa wa
Mjini Magharibi,katika mkutano wa majumuisho ya ziara aliyoifanya katika
wilaya hiyo huko Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel,Mjini Unguja
jana,(kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Baadhi
ya Viongozi wa Idara mbali mbali za Serikali wakimsikiliza, Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein,alipokuwa akizungumza na Viongozi na watendaji katika mkutano wa
majumuisho ya ziara yake.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)