MCHEZAJI PATRICK MAFISANGO ATIMULIWA SIMBA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MCHEZAJI PATRICK MAFISANGO ATIMULIWA SIMBA

SIMBA imemtimua kiungo wake wa Kimataifa Patrick Mafisango kutokana na utovu wa nidhamu.
 
Mafisango ambaye amekuwa akipewa onyo mara kwa mara na uongozi kutokana na tabia yake ya ulevi, alirudia tena kitendo hicho hivi karibuni wakati timu yake ikiwa kambini.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana toka kambi ya Simba iliyopo Bamba Beach, Mafisango baada ya kuwa 'tungi' aliporejea kambini alitoa lugha chafu kwa meneja wa timu hiyo Nichoalus Menard Nyagawa pamoja na kocha mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic kabla ya taarifa kufika kwa uongozi na ndipo mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage kuagiza atimuliwe.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages