Frans
Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi
akimwelekeza katibu mkuu Mbarak Abdulwakil katikati jinsi ya kuuweka
ufunguo wa kifaa hicho kabla ya kukirusha ndani ya kontena lenye moto,
Kushoto ni Damian George Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Your Solution
Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa nchini.
Frans
Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi akiwaelezea
wageni waalikwa mbalimbali pamoja na waandishi wa habari jinsi kifaa
hicho kinavyofanya kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak
Abdulwakil katikati akiongozana na Damian George Mkurugenzi mtendaji
wa kampuni ya Your Solution Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa
nchini kuelekea katika eneo la uzinduzi, kulia ni Kamishna wa kikosi
cha Zimamoto Kamanda Pius Nyambacha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak
Abdulwakil kulia akipokea moja ya vifaa hivyo DSPA 5 kutoka kwa
Damian George kushoto Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Your Solution
Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa nchini , wa pili kutoka kulia ni
Kamishna wa kikosi cha Zimamoto Kamanda Pius Nyambacha na anayefuatia
ni Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil
kushoto akipokelewa na Damian George kushoto Mkurugenzi mtendaji wa
kampuni ya Your Solution Limited na makamanda wa kikosi cha Zima moto,
mara baada ya kuwasili katika eneo la tukio tayari kwa uzinduzi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bw. Mbarak Abdulwakil pamoja na
Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi
inayotengeneza vifaa vya kuzimia moto vyenye teknolojia ya kisasa
vinavyoitwa DSPA 5, wakikiandaa kifaa hicho kwa ajili ya kukirusha
ndani ya kontena lililowashwa moto, ili kufunga mlango na kuruhusu
kifaa hicho kufungua gesi ya Oxgen baada ya sekunde sita tayari kuzima
moto huo ndani ya kontena hilo, tukio hilo lilikuwa ni uzinduzi wa
vifaa hivyo hapa nchini, uliofanyika katika viwanja vya Kikosi cha
kuzima moto Fire jijini Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak
Abdulwakil pamoja na viongozi wa kampuni hiyo na wakuu wa kikosi cha
kuzima moto wakishuhudia moshi mkubwa ukitoka kwenye kontena hilo baada
ya kifaa hicho kuanza kazi yake ya kuzima moto.
Askari
wa Kikosi cha kuzima mto wakiwa tayari kwa kuimza masalia madogo
madogo ya moto baada ya kifaa.Picha/Habari Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blog




No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)