BAADA YA MSOTO WA WIKI 3 WANAFUNZI UDOM WAANZA KUONYESHA FURAHA MARA BAADA YA BOOM KUINGIA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BAADA YA MSOTO WA WIKI 3 WANAFUNZI UDOM WAANZA KUONYESHA FURAHA MARA BAADA YA BOOM KUINGIA

Wanafunzi wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii wakiwa katika foleni kwenye mashine za kutolea pesa jioni hii mara baada ya pesa ya kujikimu kuingia (Boom) Sura za furaha zilianza kuonekana mara baada ya stori ya kuwa pesa zimeingia kwenye akaunti zao na ghafla foleni kwenye mashine za kutolea pesa jioni hii.

 Wanafunzi wa UDOM wakiwa katika foleni kuhakikisha kama kweli pesa imeingia jioni hii huku wengine wakionyesha nyuso za furaha ya kupata pesa baada ya msoto wa wiki tatu tokea chuo kifunguliwe.
 ATM  za CRDB UDOM,zikiwa zimeanza kufurika baada ya pesa kuwekwa jioni ya leo
Pichani Mwanafunzi Wa UDOM akimwakikishia mwenzake kuwa pesa imeingia kweli mara baada ya stori ya kuingia pesa kuanza kusikika tokea mida ya asubuhi ya leo.Hatimaye jioni hii wanafunzi hao wamewekewa pesa tayari kwa matumizi yao ya kila siku baada ya msoto wa wiki tatu tokea chuo kifunguliwe.
 Baadhi ya Wanafunzi wa UDOM wakijadiliana jambo mara baada ya pesa kuingia kwenye akaunti zao jioni hii kama kamera yetu ilivyowanasa
......................................................

Hatimaye wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma waingizia fedha zao leo jioni mara baada ya kusota kwa muda wa takriba wiki 3 sasa tokea Chuo Kifungulie.Wanafunzi hawa walikuwa wakilalamika kwanini pesa zao zichelewe kufika wakati waliasaini tokea wiki moja na nusu iliyopita wakati sharti wanatakiwa chuo kikifunguliwa wakute tayari pesa imeshaingia.
Mwanafunzi mmoja ambaye ameongea na Mtandao huu wa LUKAZA BLOG kwa sharti la kutokutajwa jina  alisema anashangaa sana kuona kwamba kwanini wamecheleweshewa pesa zao wakati walisaini muda mrefu na kusababisha wanafunzi kuishi kwa tabu sana na kusababisha baadhi ya wanafunzi wa kike kwenda kufanya umalaya kwaajili ya kupata pesa ya kujikimu.

Mwanafunzi huyu alisema kuwa pesa isingeingia kuanzia jumatatu ya leo ni kwamba wanafunzi wengi wangeishi maisha magumu zaidi na kuweza kusababisha mgomo na aliendelea kuuleza mtandao huu kuwa tokea wasaini kwaajili ya kupata pesa ni wiki na nusu sasa imepita bila kupata pesa na ndio hapo stori za kugoma zilianza kusikia chuoni na hata kwenye mtandao wa kijamii wa facebook.
 Baada ya Malalamiko ya wanafunzi hatimaye Director wa Undergraduate Studies wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alipotoa tangazo jana jumapili jioni na kuwaeleza wanafunzi kuwa pesa zao zitaingia kuanzia leo jumatatu na ndipo hapo wanafunzi walipokuwa na shauku ya kujua kama ni kweli au laaah.

Mpaka tunaenda mitamboni mtandao wa LUKAZA BLOG umeshuhudia wanafunzi wakizidi kumiminika katika mashine za kutolea pesa za CRDB jioni hii.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages