Sherehe za uzinduzi wa Kitabu cha Mh Pius Msekwa
JK akiwa na meya wa jiji la Wurzburg (shoto) na Meya wa jiji la Mwanza Jumapili jioni Ikulu ndogo ya Mwanza
Rais
Jakaya Kikwete, akiwa na Mh. Pius Msekwa wakatherehe za uzinduzi wa
Kitabu cha Mh Pius, Meya wa jiji la Mwanza, na baadhi ya viongozi
wakatia wa hafla fupi ya uzinduzi wa Kitabu cha PIUS MSEKWA,
iliyofanyika Ikulu ndogo Jijini Mwanza jana jioni. PICHA NA IKULU
UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumapili, Februari 5, 2012, amezindua Kitabu kiitwacho Uongozi na Utawala wa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere katika halfa fupi iliyofanyika kwenye Viwanja
vya Ikulu Ndogo Mjini Mwanza.
Kitabu
hicho kilichoandikwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Pius Msekwa
kinaelezea uzoefu wa miaka 25 ya Mzee Msekwa katika utumishi wa umma chini ya
uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu K. Nyerere.
Sherehe
za uzinduzi wa kitabu hicho chenye kusara 156 zimehudhuriwa na viongozi mbali
mbali wakiwamo mawaziri, viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
akiwamo Katibu Mkuu Mheshimiwa Wilson Mukama na viongozi wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza
kabla ya Mheshimiwa Rais Kikwete hajazindua kitabu hicho, Mzee Msekwa amesema
kuwa moja ya mambo yaliyomchochea aandike kitabu hicho ni pamoja na changamoto
aliyopata kuitoa Rais Kikwete kwa viongozi wastaafu wa umma kuchangia maendelea
na historia ya Tanzania kwa kuandika vitabu kuelezea uzoefu wao katika utumishi
wa umma.
Akizungumza
mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho, Mheshimiwa Rais Kikwete amempogeza Mzee
Msekwa kwa kuandika kitabu hicho na kuwataka wastaafu wengine wa utumishi wa
umma kufuata mfano wa Mzee huyo kwa kuandika uzoefu wake katika kuwatumikia
Watanzania.
Kabla
ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Msekwa ameshika nafasi nyingi za
madaraka katika Serikali na siasa ikiwa ni pamoja na kuwa Katibu wa Bunge,
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa chama cha
TANU, Mtendaji Mkuu wa CCM, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, na Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais
Kikwete yuko katika ziara ya siku tatu mjini Mwanza ambako leo alikuwa Mgeni
Rasmi kwenye Sherehe za Miaka 35 ya CCM zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM,
Kirumba.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
05
Februari, 2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)