Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi (kulia)
akizungumza na Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam
kutoka nchini Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad (kushoto) mara
baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam.
Pamoja na mambo mengine Rais huyo ameahidi kuendeleza ushirikiano kati
ya Tanzania na Iran katika sekta ya utamaduni na michezo ikiwemo
kusaidia kuleta makocha wa mchezo wa riadha.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanueli Nchimbi
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya Iran
waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Balozi
wa Irani nchini Tanzania (katikati) Movahhedi Ghomi akimweleza jambo
waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi
(kushoto) mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es
salaam. Kulia ni Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam cha
Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Benjamin Sawe na Ismail Ngayonga
Kitengo cha Habari
WHVUM.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel John Nchimbi ameishukuru Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran kwa kuanza utekelezaji wa kupatiwa kocha wa mchezo
wa riadha ikiwa ni mkataba wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Dk. Nchimbi aliyasema hayo jana (leo) alipokutana na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Dk.Mohammad Bagher Khurramshad jijini
Dar es Salaam ambapo alisema hatua hiyo ni moja ya utekelezaji wa
mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Iran.
Alisema
nchi ya Iran imekuwa ni moja kati ya nchi yenye makocha bora na wenye
uzoefu katika mchezo wa riadha kwa miaka mingi na kusema ni wakati
muafaka kuichangamkia ofa hiyo.
“Nchi
ya Iran ina makocha bora wa mchezo wa mbio za riadha sasa ni wakati
muafaka kwa Chama cha Mchezo wa Riadha kuichangamkia ofa hii ili mchezo
huu uweze kuiweka nchi katika ramani ya michezo duniani’’.Alisema Dr.
Nchimbi.
Kwa Upande wake Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Dk. Khurramshad
alisema Iran itaendelea kuisaidia Tanzania katika sekta ya
Michezo,Utamaduni na Sanaa ikiwa ni kuboresha uhusiano baina ya nchi
hizo mbili.
“Huu
ni mwanzo tu wa makubaliano ya mkataba lakini tutaendelea kuisaidia
Tanzania katika sekta za utamaduni na sanaa kama tulivyokubaliana katika
mkataba baina yetu”.Alisema Dr.Khurramshad
Serikali
ya Tanzania na Jamhuri ya Kiislam ya Iran mwezi uliopita zilitiliana
saini mkataba wa ushirikiano katika sekta za Utamaduni na Sanaa ambapo
kwa upande wa Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi na upande wa
Jamhuri ya Kiislam ya Iran iliwakilishwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Dk.Khurramshad.
Katika
mkataba huo uliosainiwa Jijini Tehran moja kati ya makubaliano ni
pamoja na ushirikiano katika sekta ya Utamaduni na Sanaa ambapo Serikali
ya Tanzania iliombwa na ilikubali kuandaa Wiki ya Utamaduni wa Tanzania
nchini Iran.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)