Nyumba hiyo iliyoezuliwa mabati (pichani upande wa kushoto) kama inavyoonekana.
Wananchi
wa Kijiji hicho wakishangilia kwa staili ya aina yake na kumpongeza
Mkuu wa Mkoa baada ya kutoa kauli hiyo, alipozungumza nao.
Mkuu wa Mkoa akiondoka eneo hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Mtonya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, waliosimama barabarani na
kuzuia msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akipita katika kijiji hicho akiwa
katika ziara yake ya Mkoa huo leo.
Wananchi
hao walifanya tukio hilo kwa ajili ya kuwataka viongozi hao kusimama na
kusikiliza kilio chao kuhusu watu waliofika kijijini hapo hivi karibuni
na kuezua mabati ya nyumba ya Mjane mwenye watoto nane, aliyefiwa na
mumewe wakidai kuwa marehemu alikuwa akidaiwa na chama cha Ushirika cha
kukopa na kulipa.
Aidha
Wananchi hao walisema kuwa watu hao walifika kijijini hapo na kuanza
kazi hiyo ya kuezua mabati na kuondoka nayo na kuiacha familia iliyokuwa
ikiishi katika nyumba hiyo ikikosa mahala pa kulala hadi hii leo
kutokana na nyumba hiyo kutokuwa na mabati.
Akizungumza
na wananchi hao Mkuu wa Mkoa, Said Mwambungu, aliwataka wananchi hao
kupunguza hasira na kuwaahidi kulishughulikia tatizo hilo kwa kuwakamata
wahusika na kuwafikisha katika mikono ya sheria na iwapo watakutwa na
hatia wataadhibiwa.
Akitoa
agizo la kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa Mkuu wa Wilaya hiyo na
Kamanda wa Polisi wa Wilaya hiyo, Mwambungu alisema kuwa, ''Tayari
nimekwisha waagiza Mkuu wa Wilaya na Kamanda wa Polisi wa Wilaya hii na
wote wapo mahala hapa, ''Mkuu wa Wilaya na Kamanda hebu simameni'',
Nawaagiza
kuanzia muda huu anzeni kazi mara moja ya kuwatia nguvuni watu hawa
waliohusika na tukio hili la ajabu na watuambie ruhusa hii ya kutesa
watu wameitoa wapi na kama waliagizwa na mahakama, Hakimu atatueleza
hukumu hii aliitoa wapi ya kuezua mabati kwa deni la mdaiwa''. alisema
Mwambungu na kushangiliwa na wananchi hao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)