VODACOM FOUNDATION YAKARABATI KITUO CHA POLISI MTO WA MBU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

VODACOM FOUNDATION YAKARABATI KITUO CHA POLISI MTO WA MBU

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha Polisi  Mto wa Mbu kilichopo  Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation kwa mara ya kwanza tangia kijengwe mwaka 1967,kwa gharama ya shilingi milioni 17.Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha  Thobias Andengenye na kulia ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya kaskazin Nguvu Kamando.
 Hichi ni Kituo cha Polisi Cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha kikionekana katika muonekano mpya baada ya kukarabatiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kiasi cha shilingi Milioni 17 kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967. 
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC) Thobiasi Andengenye akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,wakati wa hafla ya kukabidhiwa kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha , kilichokarabatiwa kwa mara ya kwanza na Vodacom Tanzania kwa thamani ya Shilingi Milioni 17 tangia kijengwe mwaka 1967.katikati ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karatu ( OCD ) Mathias Nyange.
 Mkuu wa Kituo cha Mto wa Mbu kilichopo Wilaya ya Monduli Arusha.(INSP)Amilton Matangi akiwaonyesha moja ya chumba cha mahabusu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kulia na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kushoto akisalimiana na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kaskazini Nguvu Kamando kulia wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kilichokarabatiwa na Vodacom Foundation katikati ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba akishuhudia, Jumla ya shilingi Milioni17.zimetumika katika ukarabati wa kituo hicho kwa mara ya kwanza tangu kijengwe mwaka 1967.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages