OFISI
YA RAIS IKULU-UTAWALA BORA
TAARIFA
KWA UMMA
TAMKO
LA SERIKALI KUHUSU MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP - OGP)
Tanzania
imeridhia kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazri (Open Government Partnership – OGP). Mpango huu ni juhudi za kimatifa katika
kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mkubwa wa
wananchi, kudhibiti rushwa katika jamii na kuimarisha utoaji wa huduma bora.
Vigezo
vya nchi kuwa mwanachama wa Mapango huu ni pamoja na kuandaa Mpango Kazi wa
Kitaifa (Country Action Plan) kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na
wananchi.
Kwa
kuanzia, uandaaji wa utekelezaji wa Mpango huo utahusisha vipaumbele katika
sekta tatu za Afya, Elimu na Maji ili kuimarisha uwazi, uadilifu na uwajibikaji
katika utoaji wa huduma.
Mpango
huu sasa unaboreshwa kwa kupokea maoni na ushauri kutoka kwa Wananchi na Wadau
mbalimbali. Njia za kukusanya maoni pamoja na Tovuti ya Wananchi (www.wananchi.go.tz), barua
kupitia Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu, S.L.P. 9120, Dar es Salaam, ujumbe
bila malipo kupitia simu ya mkononi (SMS) namba 0658-999222, barua pepe: ogp@ikulu.go.tz.
Mpango
Kazi wa OGP Tanzania unapatikana kwenye Tovuti ya Wananchi – www.wananchi.go.tz . Wananchi na Wadau
wengine wanaimizwa kushiri kikamilifu
kutoa maoni yao katika kuboresha Mpango Kazi wa OGP Tanzania. Mwisho wa kupokea
maoni/ushauri au mapendekezo ni tarehe 30/03/2012.
IMETOLEWA NA OFISI YA RAIS
IKULU – DAR ES SALAAM
TAREHE:.15 Februari 2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)