Mkurugenzi
wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka
akiwa na Mwanamuziki Mkongwe nchini,Mzee Hamza Kalala.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka,
akionesha vifaa vya muziki vitakavyotumiwa na Taasisi ya kuvumbua vipaji
ya Twanga Academia wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam leo.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka,
akionesha vifaa vya muziki vitakavyotumiwa na Taasisi ya kuvumbua vipaji
vya wapigaji ala za muziki ya Twanga Academia wakati wa mkutano na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kushoto ni Mhadhiri wa Chuo
Kikuu Huria (OUT), Warren Reed.
MKURUGENZI
wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka,
ametangaza kutoka kivingine kwa kuanzisha Taasisi ya kuvumbua vipaji
itakayokwenda kwa jina la Twanga Academia.
Akizungumza
na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, alisema kwamba,
Twanga Academia tayari wamenunua vifaa vyenye thamani ya sh. milioni
100 kwa kuanzia.
Aidha,
aliongeza kuwa, wamepanga kufanya usaili wa kusaka vipaji mbalimbali
vya muziki, Jumapili ijayo Februari kwenye viwanja vya Leaders Club,
kuanzia saa 6:00 mchana.
Asha
aliongeza kuwa, usaili huo, utasimamiwa na magwiji wa muziki wa dansi,
kama Hamza Kalala ‘Komandoo au Mzee wa Madongo’, Rais wa FM Academia,
Nyoshi El Saadat na wengineo kadhaa, ambako watatoa fursa kwa chipukizi
wanye uwezo wa kutumia ala za muziki.
“Lengo
la Twanga Academia, ni kusaka vipaji vya waimbaji, pamoja na
wanamuziki wenye uwezo wa kupiga ala, ambavyo vitaendelezwa kwa kupitia
wakufunzi watakaowafunda mara baada ya kupatikana,” alisema Asha.
Kwa
upande wake, Mkongwe Komandoo Kalala, alimpongeza Asha kwa hatua hiyo
aliyofikia na kwamba, ndiye atakuwa wa kwanza kukumbuka kuvumbua vipaji
vya wapigaji wa ala za muziki.
“Hiki
kitu mimi nilikuwa nakizungumzia kila siku, kwani ni wanamuziki
wachache sana, ambao wanajua kuimba na kutumia ala, wengi ni washika
vipaza sauti tu, mambo mengine hawajui, lakini hawajachelewa wanaweza
kuanza sasa, kwani elimu haina mwisho,” alisema Kalala.
Aliongeza kuwa, binafsi anamuunga mkono Asha, kutokana na kuja na wazo hilo jipya.
“Tunaliheshimu
wazo lake jipya alilokuja nalo na tutaitumia nafasi hiyo, kwa kuwapa
elimu wanamuziki chipukizi ili kuongeza tija kwa wapiga ala, tofauti na
ilivyo hivi sasa,” alisema.
Alitoa wito kwa wazazi na walezi, kuwapa ruhusa vijana wao kwenda katika usaili siku hiyo itakapofika.
Mbali
ya kusaka wanamuziki watakaomudu kupiga ala, pia watakaojitokeza
watafundishwa kuimba na kucheza, ambako zoezi hilo pia linawahusu
wasanii wa mikoani hivyo wajitokeze.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)