Mwanaharakati
wa Haki za Watoto na Afya zao Bi. Hoyce Temu akizungumza na wanahabari
kuhusiana na kampeni ya kupambana na utapiamlo kwa watoto, ambapo
amesema tatizo hilo ni kubwa sana hapa nchini na kuishauri serikali
ielimisha jamii umuhimu wa kula chakula bora na pia kutoa ufafanuzi kuwa
chakula bora ni kipi.
Dr.
Ellen Otaru Okoedian akitoa mwongozo kwa wawakilishi wa mabaraza ya
Wanafunzi kutoka wilaya za jiji la Dar es Salaam wakati Shirika la Save
the Children lilipofanya uzinduzi wa taarifa ya Lishe leo jijini Dar es
Salaam.
Wanafunzi
wakiwa makundi kuandika mapendekezo wanayodhani yakifanyiwa kazi na
Serikali yatasaidia kuhamaisha mpango wa kupambana na Utapiamlo kwa
watoto.
Makundi ya Wanafunzi hao katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge na waandaaji wa uzinduzi huo.
·MDAU WA HAKI ZA WATOTO HOYCE TEMU ASHAURI ELIMU YA LISHE ITOLEWE KWA WANANCHI.
Shirika la Save the Children Tanzania limesema licha ya kuwepo
maendeleo, watoto wanne kati ya kumi wenye umri wa miaka isiyozidi
mitano nchini Tanzania wamedumaa.
Katika
muhtasari wa wa hali ya Tanzania inaonyesha asilimia 17 wameathirika
sana na kila siku watoto 130 wanakufa kutokana na magonjwa yanayohusiana
na utapiamlo.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa lengo la Milenia namba 4 linalotaka kupunguza
theluthi mbili ya vifo vya watoto haliwezi kufikiwa bila kukabiliana na
utapiamlo.
Akizungumza
wakati wa hafla ya chakula baada ya kuzinduliwa kwa kampeni hiyo,
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mh. Lediana Ng’ong’o ambaye ni
mwanaharakati wa masuala ya lishe ameshauri serikali kuajiri wataalam wa
lishe ikiwezekana katika kila wilaya nchini.
Naye
Mdau wa Kuhamasisha Haki za Watoto na Afya zao Hoyce Temu aliyealikwa
katika uzinduzi huo, amesema ni muhimu serikali ikatoa elimu ya lishe
kwa wananchi, ili waweze kutambua umuhimu wa kula chakula bora na faida
zake kimwili na kiakili.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)