Wakiwa katika picha ya pamoja.
KATIKA
kukabiliana na tatizo la maji nchini RoratyClabu Tanzania inatarajia
kutumia dola za kimarekani zaidi ya milioni moja mwaka ujao kwa ajili ya
kutekeleza mradi wa tekinolojia ya kisasa ya kuchimba visima pamoja na
kusambaza maji katika maeneo yenye uhaba.
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa Rotary Clabu Tanzania Harish Bhatt, kwenye
mkutano wa tatu wa mwaka uliofanyika jijini Dar es Salaam, ukiwa na
lengo la kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya mwaka ujao.
Aidha
alisema, tayari mradi wa maji ulishaanza kwa kusambaza maji katika
shule 20 za mkoa wa Dar es Salaam na kwamba ni matumaini yao kwa mwaka
ujao wataenda kwenye maeneo yasio na maji kwa lengo la kuhakikisha
tatizo linapungua kama si kuisha kabisa.
Alisema
kwa sasa rotary clabu ina malizia mradi wa kujenga wadi ya watoto
wanaosumbuliwa na magonjwa ya saratani katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili pamoja na miradi mingine ya kimaendeleo kote nchini.
Mradi
wa maji kwa mwaka ujao ni makubaliano ya Rotary clubu zote za Afrika
kuwa pamoja na miradi mingine ya maendeleo maji yatapewa kipaumbele cha
kwanza.
"Maji
imekuwa ni tatizo kubwa hivyo kupitia clabu zetu tutaandaa marathoni
nyingine kwa lengo la kukusanya pesa kwa ajili ya mrdia mkubwa wa maji
mwakani utao tumia tekinolojia ya kisasa mkutano huu ambao hufanyika
mara moja tu mwaka unalengo la kujua ni wapi tumekosea pamoja na
kubadilishna mawazo na kupanga mikakati yetu" alisema.
Akifungua
mkutano huo Gavana Mteule kutoka nchi tano za Afrika Geeta Manek
alishukuru Tanzania kwa kuendeleza amani nchini na kuwa na moyo wa
kujitolea kwa ajili ya wengine tofauti na nchi nyingine.
Alisema
rotary haina udini wala ukabila kila mwenye vigezo anaweza kujiunga
kwa lengo la kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali ikiwa ni malengo
makuu ya kuanzishwa kwa clabu hiyo kote duniani.
Gavana huyo mteule ambaye amesisitiza amani ncini anawakilisha nchi za Kenya, Uganda, Elitrea, Tanzania na Ethiopia.
Kwa
upande wake Katibu wa Rotary Clabu Mkoa wa Rukwa Daniel Mtweve
alishukuru watanzania kwa kuondoa dhana potofu ya kudhani rotary ipo kwa
ajili wa wahindi peke yako badala yake wamejiunga kwa wengi.
Alisema
kwa sasa mkoa wa Rukwa baadhi ya wakazi wameshafaidika na miradi yao
inayoendelea ukiwemo ule wa kusaidia madawati kwa watoto wa shule.
Mkutano
huo wa siku moja uliandaliwa na Rotary Club ya Dar es Salaam ambapo
jumla ya wanachama 200 walishiriki kwa lengo la kubadilishana mawazo na
uzoefu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)