Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Mahakama ya Rufaa Tanzania
,kuhusu siku ya sheria nchini itakayofanyika kesho jiji Dares
Salaam.Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa Tanzania , Francis Mutungi.
baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kati yao na Jaji Mkuu
wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (ambaye hayupo pichani ) kuhusu siku
ya sheria nchini itakayofanyika kesho jijini Dares Salaam.
---
NA ZAWADI MSALLA- MAELEZO
2/2/2012
RAIS Jakaya
Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya
sheria nchini, yatakayo fanyika kitaifa katika viwanja vya Mahakama ya
Rufaa jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa habari jana Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande
Othman alisema maadhimisho hayo yamelenga katika kujadili masuala
mbalimbali ya kisheria ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi kwa
ujumla.Jaji Mkuu aliongeza kuwa wananchi wengi wanapoteza haki zao za
msingi kwa kutokujua sheria, hivyo kuna umuhimu wa kujua aina za makosa
na adhabu zinazoweza kutolewa katika makosa hayo.
“Tangu
kuanzishwa kwa sherehe hizi, zimelenga zaidi katika kuhakikisha
wananchi wanajua mambo mbalimbali ya kisheria yanayowahusu kwani wengi
huwa wanapoteza haki zao za msingi kwa kutokujua sheria, kutokujua
sheria haina msamaha katika kosa.” alisema Jaji Mkuu.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni adhabu Mbadala katika kesi za Jinai:
Faida zake katika jamii.
Shereha
hizo pia zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Spika
wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na Rais wa chama cha Mawakili nchini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)