Precision Air – Shirika
la ndege linaloongoza Tanzania imenyakua tuzo ya Shaba baada ya kushika nafasi
ya tatu katika mashindano ya shirika bora la ndege Afrika kwa mwaka 2011/2012, yaliyoendeshwa
na ‘African Aviation News Portal’.
Mara baada ya kupokea
taarifa hizo, Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Bw. Alfonse Kioko alisema, “Kutambuliwa na
wateja wetu pamoja na washindani wetu ni heshima kubwa sana. Kushika nafasi ya
tatu Afrika si jambo dogo. Napenda kuwadhibitishia wateja wetu kwamba
tunaendelea vyema na mipango yetu ya kupanuka kibiashara na kuwahakikishia pia huduma
bora yatakayopita mategemeo yao.”
Kwa mujibu wa African Aviation kura zilizopigwa na
wasomaji wake, wataalam wa masuala ya anga, na wasafiri wa ndege wa mara kwa
mara “zimeangalia ukuaji mzima wa kampuni, huduma kwa ujumla, pamoja na sifa na
uhakika wa huduma za kampuni.”
Precision Air imeshika
nafasi ya tatu nyuma ya Ethiopian Airlines iliyoshinda nafasi ya kwanza na
kuzawadiwa tuzo ya Dhahabu ikifuatiwa na Kenya Airways (wapili) walioshinda
tuzo ya Fedha.
Kura zilipigwa kutumia njia ya mtandao katika tovuti hiyo,
pamoja na kupiga kura za moja kwa moja katika vikao, makongamano, na matukio
mbali mbali yaliyoshirikisha shirika hilo la African Aviation. Zaidi ya wapiga
kura 20,000 walishiriki.
Jumla ya mashirika ya
ndege zilizoshiriki mashindano hayo yalikuwa 25; Air Algerie, Air Botswana, Air
Malawi, Air Namibia, Air Nigeria, Air Uganda, Arik Air, Asky Airlines.
Wengine ni; Camair-Co,
Comair South Africa, Dana Air, Egyptair, Ethiopian Airlines, Fly540, Kenya
Airways, Mozambique Airlines, Precision Air, Royal Air Maroc, Rwandair, Senegal
Airlines, South African Airways, Sudan Air, TAAG Angola, TACV and Zambezi
Airlines.
African Aviation, pitia
wasomaji na wafuatiliaji (followers) wake, wanatambua mashirika yenye maendeleo
yaliyojizatiti katika huduma bora kwa wateja, utaalamu, ubunifu na kuchangia mafanikio
katika sekta ya utalii Afrika. Tuzo hii “si tu kipimo
cha mafanikio ya mashirika ya ndege bali pia ni ishara ya kuridhishwa kwa
wateja katika sekta zote za usafiri wa anga,” inasoma kipande cha taarifa
kutoka tovuti ya African Aviation.
Katika miaka ya hivi
karibuni shirika la Precision Air limeweza kunyakua zawadi zifuatazo; ‘Best
Scheduled Domestic Airline in Tanzania’ kwa mwaka 2011 iliyozawadiwa na Umoja
wa Wakala wa Tiketi za ndege Tanzania (TASOTA); ‘Regional Airline of the Year’
iliyotolewa na Asasi ya Mashirika ya ndege Afrika (AFRAA ) 2010; ‘CEO’s Most
Respected Company in Tanzania’ iliyofanyika
kwa utafiti wa Pricewaterhouse Coopers
kwa ukanda wa Afrika Mashariki 2008/9; ‘African Deal of the Year -2008’
iliyotolewa na Jarida la Airfinance kwa ajili ya mkataba wa dola 129 milioni
ziliwezesha Precision Air kupata ndege 7 mpya aina ya ATR; pamoja na ‘Aircraft
Leasing Deal of the Year in Africa- 2008’ iliyozawadiwa na jarida la Jane's
Transport Finance kwa ajili ya mkataba huo huo wa ndege mpya 7.
Tayari African Aviation
imeanza tena mchakato wa kutafuta Shirika bora la ndege la Kiafrika kwa mwaka
2012/2013, kwa yeyote anayependa kushirika kwa kupigia kura shirika letu la
ndege la Precision Air anaweza tembelea tovuti ifuatayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)