Mwenyekiti
wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiwa meza kuu na Rais wa Zanzibar Dkt
Mohamed Ali Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na Rais Mstaafu
wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili
Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mh Pius Msekwa
na Katibu Mkuu wa CCM Mh Wilson Mkama kabla ya kuanza kwa mkutano wa
Halmashauri Kuu leo katika jengo la White House la Makao Makuu ya chama
hicho mjini Dodoma leo February 12, 2012
Picha na IKULU Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi imefanya kikao chake maalum chini ya mwenyekiti wake wa taifa dr. Jakaya mrisho kikwete tarehe 12.02.2012. Katika kikao hicho halmashauri kuu ya taifa pamoja na mambo mengine imeamua;Taarifa kwa vyombo vya habari
Utangulizi:
Kufanya marekebisho ya katiba ya ccm ya 1977, toleo la 2010 na kanuni zake.
Halmashauri kuu ya taifa imeridhia marekebisho ya katiba ya CCM ya 1977, toleo la 2010 hivyo kubadili namna ambavyo wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa inavyopatikana.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM watakuwa katika makundi yafuatayo:-
(a) ngazi ya taifa
wajumbe 10 kutoka tanzania bara
wajumbe 10 kutoka tanzania visiwani
(b) wajumbe 10 wa kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM taifa
(c) wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao.
(d). Wajumbe wanaotoka kwenye vyombo vya uwakilishi
i. Wanaochaguliwa na bunge 10 (bara 8, zanzibar 2)
ii. Wanaochaguliwa na blw 5 (zanzibar 5)
(e). Wajumbe wanaochaguliwa kutoka wilayani.-221
wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa waliochaguliwa kupitia wilaya watakuwa ni viongozi wa kazi za muda wote ili kuweka wazi zaidi wajibu wa wajumbe hao wa kuwa karibu na wanachama na kushughulikia shida zao.
(f). Wajumbe toka kwenye jumuiya za chama
i. Wanaochaguliwa na uwt 15 (bara 9, zanzibar 6)
ii. Wanaochaguliwa na uvccm 10 (bara 6, zanzibar 4)
iii.wanaotokana na wazazi 5 (bara 3, zanzibar 2)
Aidha halmashauri kuu ya taifa imeamua kuwa viongozi wakuu wastaafu ngazi ya taifa waundiwe baraza la ushauri.
Baraza hilo litakuwa na wajumbe wafuatao:-
• marais wastaafu wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambao walikuwa wenyeviti wa ccm taifa.
• marais wastaafu wa zanzibar ambao pia walikuwa makamu wenyeviti wa ccm taifa.
• makamu wa mwenyekiti wa ccm taifa wastaafu.
Baraza litakuwa na kazi ya kutoa ushauri kwa chama cha mapinduzi na serikali zinazoongozwa na ccm, kwa madhumuni hayo hayo katika jambo mahsusi. Wajumbe wa baraza hilo wanaweza pia kualikwa ama wote au mwakilishi wao kuhudhuria vikao vya chama ngazi ya taifa.
Imetolewa na:
Nape M. Nnauye.
Katibu wa NEC wa itikadi na uenezi





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)