Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akizungumza Wilayani
Mpanda. Kushoto ni Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal na
Mke wake Mama Asha Billal.
NA HAMZA TEMBA-OFISI YA MKUU WA MKOA
rukwareviw.blogspot.com
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ameiomba Serikali kupitia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed
Gharib Billal kusaidia kuhakikisha ujenzi wa barabara za lami
zinazoendelea kujengwa Mkoani Rukwa zinakamilika kwa wakati.
Mkuu
huyo wa Mkoa alitoa ombi hilo jana mara baada ya kusomwa taarifa ya
ujenzi wa barabara za lami zinazoendela kujengwa Mkoani humo kwa Mhe.
Makamu wa Rais ambapo taarifa hiyo ilielezea changamoto zinazokabili
ujenzi huo ambazo zinatishia kukamilika kwa ujenzi huo katika muda
uliopangwa.
Taarifa
hiyo iliyowasilishwa na Meneja wa Tanroads Mkoa wa Rukwa Ndugu Florian
Kabaka jana iliweza kuainisha changamoto mbalimbali zinazoukabili
ujenzi huo ikiwemo ucheleweshwaji wa malipo ya fedha kwa ile miradi
inayotemea fedha za ndani hususani barabara za Sumbawanga-Kasanga na
Sumbawanga-Mpanda.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo changamoto nyingine ni baadhi ya wakandarasi
wanaojenga barabara hizo kukimbiwa na wafanyakazi wao kutokana na
ukosefu wa fedha za kuwalipa hali inayopelekea kuzorota kwa ujenzi huo.
Mbali
na changamoto hizo, nyingine ni kuchelewa kulipwa fidia wananchi
waliothibitika kustahili malipo hayo ili kuepusha shughuli za ujenzi
katika maeneo wanayotakiwa kuhama.
Pamoja
na changamoto hizo nyingine ni wizi wa vifaa vya ujenzi wa barabara
hizo zikiwepo nondo, mafuta, simenti, vyuma na hata mabati. Kwa mujibu
wa Meneja huyo wa Tanroads ujenzi huo unatakiwa kukamilika mwakani 2013
lakini kama hali itaendelea kuwa hivyo basi huenda ukamilishaji wa
miradi hiyo ukachelewa.
Baada
ya kusomwa taarifa hiyo ilifika wakati kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
kumkaribisha na kumtambulisha Mhe. Makamu wa Rais kwa wananchi wa
Wilaya ya Nkasi ambapo amenza ziara akitokea Wilayani Mpanda. Kabla ya
kufanya hivyo alilazimika kutumia fursa hiyo kutoa ombi lake rasmi kwa
Makamu wa Rais kuhusu ujenzi unaondelea na kuhakikisha kuwa changamoto
zinzozikabili barabara hizo zinapatiwa ufumbuzi.
"Wananchi
wote wa Mkoa wa Rukwa wanaishukuru sana Serikali yao kwa hatua yake
kubwa ya kuleta miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za lami Mkoani
hapa kitu ambacho ni cha kujivunia kwa wanarukwa wote, Nitumie fursa
hii kuiomba Serikali itusaidie kuondokana na changamoto zinazoikabili
miradi hii ili iweze kuakamilika kwa wakati" Alisema Injinia Manyanya.
Serikali
imesaini mikataba ya ujenzi wa barabara za lami Mkoani Rukwa kwa
barabara za Tunduma-Ikana-Laela, laela-Sumbawanga, Sumbawanga-Kasanga
na Sumbawanga-Mpanda. Hadi hivi sasa ujenzi wa barabara kwa baadhi ya
maeneo hayo unaendelea na maeneo mengine yamesimama kwa muda kutokana
na uhaba wa fedha.
Mhe.
Makamu wa Rais yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku saba
ambapo, ameshatembelea Wilaya ya Mpanda, Sasa yupo Wilayani Nkasi na
baadae atamalizia ziara yake Wilayani Sumbawanga amabap atatembelea
miradi mbalimbali ya maendeleo, kuizindua na kuweka mawe ya msingi.
Ziara yake hiyo itakamilika tarehe 24 Februari 2012 ambapo ataenda Mkoa
jirani wa Mbeya kwa ziara kama hiyo ya kikazi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)