MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MKOANI RUVUMA KUANZA ZIARA YA SIKU NNE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MKOANI RUVUMA KUANZA ZIARA YA SIKU NNE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mkoa wa Ruvuma, Delphin Fredrick, ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa vyama vya upinzani waliohudhuria mapokezi ya Makamu wa Rais alipowasili mkoani Ruvuma jana Febriari 14,2012 kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku nne. Viongozi wengine wa Upinzani waliokuwapo ni pamoja na Katibu (W) Songea mjini wa Chama cha CUF, Mohmed Makoma, Katibu wa TLP Mkoa Ruvuma, Wellnery Methody Kilowoko na Mwenyekiti wa (W) Songea Mjini TLP, Elias Nchimbi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Said Thabit Mwambungu, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mkoani humo kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku nne jana Februari 14, 2012. Akiwa mkoani Ruvuma, Dkt Bilal atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi katika baadhi ya miradi ya mkoa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mbunge Vita Kawawa, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mkoani Ruvuma jana Februari 14, 2012 kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku nne katika mkoa huo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akifurahia ngoma ya asili wakati wa mapokezi yake kwenya uwanja wa ndege wa mkoani Ruvuma jana Februari 14, 2012 alipowasili kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku nne mkoani humo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages