Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Afungua Mkutano wa Kwanza wa Hali Ya Siasa Zanzibar - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Afungua Mkutano wa Kwanza wa Hali Ya Siasa Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaojadili HALI YA SIASA ZANZIBAR huko hoteli ya Bwawani. Mkutano huo umeandaliwa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) ulio chini ya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokea nakala ya kitabu cha Mkutano wa kwanza wa hali ya siasa Zanzibar uliofanyika mwaka 2009, pamoja na machapisho mengine ya REDET kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala, mara baada ya kufungua mkutano wa pili wa hali ya siasa Zanzibar huko hoteli ya Bwawani
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiongozana na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa REDET unaofanyika hoteli ya BWawani Mjini Zanzibar.Picha na Salmin Said-Ofisi Ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages