Waziri
wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli (MB) leo
ametoa taarifa ya pamoja na Balozi wa Japan hapa nchini Mh. Masaki
Okada iliyohusu Mradi wa Upanuzi wa barabara ya Kilwa kwa Awamu ya pili.
Akizungumza
na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mh. Magufuli ameelezea hatua
iliyochukuliwa na Wizara yakekwa Pamoja Balozi wa japan ya kuunda
Kikosi Kazi cha Pamoja kilichochunguza kuharibika mapema kwa barabara ya
Kilwa hasa katika sehemu iliyojengwa katika Awamu ya Pili ya Mradi huo.
Aidha amefafanua kuwa mpango wa Mkandarasi wa kuanza matengenezo ya barabara hiyo ni mwezi Mei 2012 baada ya kipindi cha mvua.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)