Ofisa Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba
kushoto akipokea zawadi ya mbuzi toka kwa baadhi ya wazazi wa
wanafunzi wa shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo mkoani pwani,mara
baada ya kuwakabidhi rasmi vyumba vitatu vya madarasa na madawati 100
kwa ajili ya shule hiyo,Msaada huo uliotolewa na Vodacom Foundation
umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 98.
Haya ndiyo madarasa ya shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani yaliyojengwa na Vodacom Foundation.
Mkurugenzi
wa Wizara ya Elimu shule za Msingi,Zuberi Samataba mwenye suti
akiongea jambo na 0fisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania
Mwamvita Makamba,walipowasili katika shule ya msingi ya Ruvu Darajani
iliyopo Mkoani Pwani kwa ajili ya kukabidhi msaada wa madarasa matatu
na madawati 100 uliotolewa na Vodacom Foundation katika shule hiyo na
kugharimu zaidi ya shilingi Milioni 98.
Hili
ndilo jiko la wanafunzi wa shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo
Mkoani Pwani,Taswira hii imepigwa na mpiga picha wetu katika
makabidhiano ya vyumba vitatu vya madarasa pamoja na madawati 100
vilivyokabidhiwa rasmi mwishoni mwa wiki na Vodacom Foundation kwa
ajili ya shule hiyo,wadau jitokezeni msaidie hata kujenga jiko hilo.
Kikundi
cha ngoma cha wazazi wa mkoa wa Pwani wakitumbuiza wakati wa
makabidhiano rasmi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na madawati 100
vilivyokabidhiwa rasmi mwishoni mwa wiki na Vodacom Foundation kwa
ajili ya shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani,Msaada
huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 98,
0fisa
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba,
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja
na madawati 100 vilivyokabidhiwa rasmi na Vodacom Foundation kwa ajili
ya shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani,Msaada huo
umegharimu zaidi ya shilingi milioni 98,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
shule za msingi Wilaya ya Bagamoyo na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule
hiyo Mary Nzowa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)